Pwani, Tanzania. Kuna taarifa kuwa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani imekutana hivi punde wilayani Bagamoyo na kufanya kikao cha kuandaa mashitaka ya kisheria dhidi ya Mwenyekiti huyo wa Chadema, Freeman Mbowe kutokana na kufanya mkutano wa hadhara kinyume cha utaratibu.
Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kwa mara nyingine tena amevunja sheria kwa kufanya mkutano wa hadhara katika eneo la Magomeni wilayani Bagamoyo LEO saa 4:00 asubuhi.
Ratiba ya Kampeni za Uchaguzi wilayani humo inaonyesha kuwa leo tarehe 1/2/2014 ni zamu ya Chama cha Wananchi (CUF) kuendesha kampeni zake.
Juzi Mbowe aliwekwa katika kituo cha polisi kwa saa kadhaa baada ya kuvunja sheria ya mkutano wa hadhara mkoani Iringa.
Kutokana na hali hiyo tayari kamati ya Siasa ya Mkoa wa Pwani imekutana hivi sasa wilayani bagamoyo na kufanya kikao cha kuandaa mashitaka ya kisheria dhidi ya Mwenyekiti huyo wa Chadema.