Tamko la hamis Mgeja mwenyekiti wa CCm, Mkoa wa Shinyanga juu ya Edward Lowassa...

 Kitendo alichokifanya hivi karibuni Ndugu Paul Makonda Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji pale alipoongea na vyombo vya Habari pamoja na mambo mengi aliyoyaongea kubwa zaidi ni alipotamka wazi kwa kuwatuhumu baadhi ya Viongozi wa Dini kwa kutoa maneno ya kejeri na dharau dhidi yao kuwa “MASHEIKH NA MAASKOFU WAKIWEMO NA VIJANA WANAOTAKA FEDHA ZA BURE WAENDE KWA EDWARD LOWASA” kitendo ambacho hakuwatendea haki wala adabuViongozi hawa wa Dini.
Kitendo hicho cha kuwakejeri na kuwadhalilisha ni utovu
wa Nidhamu wa hali ya juu sana, kwani
kauli aliyoitoa kila
Muumini ilimshitua sana, kwani ni kauli
haikupaswa
kutolewa na Kiongozi wa Vijana aliyekuwa katika nafasi
Muhimu ya Uongozi wa Jumuiya Kitaifa,
kwani kauli yake
hiyo yenye ukakasi wa hali ya juu sana
imempa
kichefuchefu kila mmoja anaewaheshimu Viongozi wa Dini,
kwani Viongozi wa Dini wanaheshima
zao binafsi na
kuheshimika Duniani kote na mpaka
Serikali huwaomba
Viongozi wa Dini kushiriki pamoja kutatua na kushauriana
katika maswala mbalimbali
yanayoizunguka jamii.
Kauli hiyo ni nzito sana aliyoitoa Ndugu
Paul Makonda sio
ya kuipuuza hata kidogo na kuicha hivi hivi nina muomba
kwa Heshima na taadhima Mwenyekiti wa
Vijana wa Taifa
awathibitishie Watanzania kuwa kauli
aliyoitoa Ndugu Paul
Makonda ni ya Umoja wa Vijana au ni yake binafsi. Kwani
mimi binafsi nimekuwa katika Umoja wa
Vijana kama
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Shinyanga
mstaafu na
Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana Taifa lakini pia
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Umoja
wa Vijana Taifa,
nafahamu kauli au matamko mazito
kama yaliyotolewa na
Ndugu Paul Makonda hutolewa na Mkutano mkuu wa Taifa,
Mkutano wa Baraza Kuu Taifa na hata
kamati ya
Utekelezaji Taifa.Mimi siamini kama hiyo
ni Kauli ya Umoja
wa Vijana kwa kadri ninavyofahamu utaratibu ndani ya
Jumuiya na Chama kwa ujumla, sasa
tunajiuliza huyu
kijana kauli hizi nzito nzito ambazo
hazilingani na umri
wake na wala hadhi ya kiuongozi aliyonayo anazitowa
wapi huenda tunaamini kuna kundi au
genge la
mahafidhina liko nyuma yake lililoamua
kumtumia aidha
kwa kujua au kwa kutokujua. Jambo jingine muhimu alitutuhumu pia
sisi yani mimi
Khamis Mgeja, Mzee Mgana Msindai na
Ndugu John
Guninita kuwa alidai t--------- na Ndugu
Edward Lowasa, tuhuma hizi si za kweli hata kidogo
napenda Watanzania
wafahamu tuhuma zote mbali mbali
ambazo kijana huyu
amekuwa akitushutumu si za kweli na ni
za kipuuzi ninaiomba jamii kumpuuza kwani Ndugu
Makonda bado
mchanga kisiasa anatafuta umaarufu kwa
kasi kwa
kutumia migongo yetu sisi wakongwe
kisiasa, kwani sisi aliotutuhumu atambue sisi ni wakongwe
na ni Magwiji
katika siasa za kiungwana hapa Tanzania,
tunauwezo wetu
binafsi wa kufikiri na kuamua kile
tunachokiamini kwa maslahi ya Chama na Taifa kwa ujumla,
kwa ujumla
tunataka Ndugu Paul Makonda na
washirika wake waache
kelele ambazo wamekuwa wakilalamika
mara kwa mara hii ni dalili ya kuelemewa ndio maana
hawaishi kumsemasema
na kumkejeri Ndugu Edward Lowasa
wakati ambapo jamii
inamuona kuwa ni mtu wa msaada
mkubwa katika kuchagiza maendeleo kwa kushirikiana
na jamii. Kijana
Makonda atambue sisi tumewekeza jasho
jingi katika
chama hiki na kamwe hatutokubali
kudhalilishwa na kijana mchanga wa kisiasa kama huyu, pia kama
ni kuwekeza
jasho sisi tuna debe ishirini yeye hata
robo hajafikisha
katika medani za kisiasa kwa hivyo
anafanya maajabu ya kisiasa ni maajabu ya panya kufukuza
paka na anacheza
ngoma asiyoijuwa.Pia jamii inamuona
Ndugu Edward
Lowasa ni mtu muungwana, mwenye
uwezo mkubwa wa kiutendaji, mwenye ushauri na ushawishi
mkubwa katika
machangizo ya maendeleo, sifa kubwa
nyingine ya ziada ni
uvumilivu na hasa kuwavumilia watu
wenye kumrushia madongo kama Paul Makonda na genge
lao la mahifidhina.
Kuhusu kauli aliyoitamka Ndugu Makonda
ya kwamba
Ndugu Edward Lowasa hawezi kuwa Rais
kauli hii imetoa picha ya kuyajuwa yaliyofichika katika
fikra za kundi hili la
wahifidhina lakini pia watambue
maamuzi yote hufanywa
na Vikao halali vya chama na jumuiya
zake, na wakati ukifika vikao vitaamua na si Makonda na
marafiki zake.
0.2 MZEE MALECELA KUPONGEZA KAULI ZA
KASHFA
DHIHAKA NA KEJERI DHIDI YA VIONGOZI
WA DINI Kufutia tukio la hivi karibuni la kijana Paul
Makonda kutoa maneno
ya kashfa kejeri na dhihaka dhidi ya
viongozi wa Dini,
baadhi ya wanasiasa na vijana maaajabu
makubwa kutokana na kauli hizo za Makonda
tumemshangaa Mzee
Malecela kuibuka na kuunga mkono na
kumpongeza kijana
huyu mtovu wa nidhamu.
Tulitegemea kila Mtanzania kwamba baada ya kauli hizo
Mzee Malecela angeibuka na kumuongoza
njia sahihi na
kumpa ushauri kijana huyu aliyepotea
kimaadili wa kwenda
kuwaomba radhi na kuwaangukia viongozi wa Dini, ndugu
Edward Lowasa, Ndugu Khamis Mgeja,
Ndugu Mgana
Msindai, Ndugu John Guninita ikiwemo na
vijana kwa
ujumla.Maajabu makubwa jambo ambalo Watanzania
hawakutegemea jinsi wanavyomfahamu
Mzee Samwel
Malecela na heshima yake, tulitaraji kuwa
Mzee
angemkemea kijana huyu mtovu wa Nidhamu badala yake
anampongeza na kumuunga mkono na
kuwataka
Watanzania wamuunge mkono kwa kauli
zake za utovu wa
Nidhamu ambazo hazina tija kwa Chama na maendeleo ya
Taifa kwa ujumla, pia katika maajabu
mengine Mzee
Malecela alimshambulia mwanachama
mwenzake Ndugu
Edward Lowasa kwa kumtuhumu kwa tuhuma nyingi
mbalimbali ambazo hana ushahidi
nazo.Mzee Malecela
amesahau huko nyuma yeye alishawahi
kutuhumiwa kuwa
alipewa fedha kutoka nchi za uarabuni na mpaka
kubadilisha dini na kuitwa jina la
JUMANNE ili aungwe
mkono kupewa nguvu za kugombea Urais.
Kuhusu uchu wa Urais anaomtuhumu
Ndugu Lowasa amesahau yeye ndiye ana uchu mkubwa
sana wa
Madaraka alikuwa akiomba nafasi za
ndani ya Chama
haswa kwa kiti cha Urais kwa awamu
mbalimbali akaonekana hafai na hatoshi na mpaka
jina lake likawa
halipitishwi na chama baada ya
kumgundua ni dhaifu na
anakasoro kubwa za kimaadili na mpaka
ikapelekea Baba wa Taifa akachoka kumvumilia na
hatimae alimtungia
kitabu “UONGOZI WETU NA HATIMA YA
TANZANIA” hii ni
kuonyesha kuwa Mzee Malecela alikuwa
sugu wa matatizo yaliyokuwa yakikiuka maadili.Jambo
jingine alilokuwa nalo
la uchu wa madaraka Mzee Malecela ni
pale
alipong’ang’ania kiti chake cha ubunge
bila kujali umri wake na wananchi wa jimbo la Mtera
ilifika mahala
walimchoka baada ya kugundua anasinzia
Bungeni na
kwenye jimbo laketulishuhudia Kibajaji
kikiliangusha Katapila maana yake aliangushwa ubunge
na mtoto mdogo
Mhe Livingstone Lusinde.Jambo jingine
Mzee Malecela
ameshindwa kutambua wanaokivuruga
chama ni wale wanaozungumza nje ya vikao halali vya
chama na jumuiya
zake na kuyageuza kuwa ndio msimamo
wa chama au
jumuiya.
Kwa hivyo Mzee Malecela kuendelea kutushambulia
hatutendei haki kwani hakuna shughuli
yoyote ya chama
iliyokwama kuanzia ngazi ya tawi hadi
taifa kwa sababu
yetu sisi.NINAPENDA KUTOA USHAURI KWA MZEE
MALECELA, MAKONDA NA WATANZANIA
WENZANGU KWA
UJUMLA, Tanzania kama taifa tumefika
pabaya kwani kila
mmoja amebaki kuwa mlalamikaji na kutuhumiana
pasipokuwa na ushahidi hili jambo ni
hatari kwa
mustakbali wa nchi kwani hivi sasa
baadhi ya watu
wanamgeuza Ndugu Edward Lowasa kuwa ni agenda ya
kitaifa huku wakiacha mambo muhimu ya
nchi na maisha
ya watanzania.kwani tulitegemea wazee
wetu kama kina
Mzee Malecela watushauri vipi taifa linaweza kukabiliana
na changamoto zilizopo hivi sasa kwa
mfano deni la taifa,
mchakato wa Katiba Mpya, matatizo ya
umasikini, tatizo la
ajira kwa vijana, hombwe kubwa kuwahi kutokea baina
walionacho na wasionacho, mauaji
yanayotokea sasa
maeneo mbalimbali kati ya wakulima na
wafugaji ikiwemo
kuchomeana nyumba, mauaji ya kikatili kule Tarime na
maeneo mbalimbali nchini, ajali mbali
mbali za barabarani
zinazouwa nguvu kazi ya Taifa, tatizo
kubwa la rushwa,
uporaji wa rasilimali za Taifa na ujangili wa kutisha,
Tanzania kutumika kama korido la
kupitishia madawa ya
kulevya na binadamu, oparasheni
tokomeza, wananchi
kujichukulia sheria mkononi, ubadhilifu wa mali za umma
haswa ukizingatia ripoti ya mkaguzi
mkuu wa hesabu za
serikali na taarifa za kamati mbalimbali
za bunge, jambo
jingine kubwa lilipo kwa sasa ni kuhusu rasilimali ya gesi
iliyovumbuliwa kwa wingi nchini wakati
taifa lipo katika
mchakato wa kutunga sera na sheria ya
gesi na mafuta.
Mzee Malecela na wenzake hayo yaliyotajwa hapo juu ndio
mambo muhimu yanayogusa nchi na sio
mtu Lowasa
Lowasa Lowasa tulitegemea atushauri
Tanzania kama taifa
tufanye nini Watanzania kwa kushirikiana na Serikali yetu
kwani matatizo hayo yanahitaji
ushirikishwaji baina ya
wananchi na Serikali yao, Watanzania
wangeyapata hayo
kupitia uzoefu wake kama alivyowahi kuwa Makamu wa
Rais, Waziri Mkuu, Makamu wa
Mwenyekiti wa CCM kuliko
maajabu ya kuonyesha Flana yenye
maneno ya “FRIENDS
OF LOWASA” kuwa kama ndio tatizo la Taifa.
Mzee Malecela kuwaonyesha Watanzania
Flana ya Lowasa
ndio tatizo la taifa hii inaonyesha wazi
Mzee amechoka na
amefilisika kifikra na anazeeka vibaya ninapenda nimpe
ushauri wa bure Mzee wangu atulie alinde
heshima
yake.Pia napenda nitoe ushauri kwa Mzee
Malecela, Paul
Makonda pamoja na washirika wao wasome alama za
nyakati na waangalie mahitaji ya siasa
kwa sasa na waone
Watanzania wanamuhitaji Kiongozi wa
namna gani wa
Tanzania ya kesho, ninawaomba wakubali yaishe wasije
kupinganaTanzania na nguvu ya umma na
upepo wa kisisa
kwa sasa na pia watambue mpaji ni
MUNGU alitakalo
MUNGU hakuna mwanadamu atakaelizuia. NAWATAKIA KILA LA HERI KATIKA UJENZI
WA TAIFA
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU
WABARIKI
WATANZANIA
TAARIFA HII IMETOLEWA NA NDG KHAMIS MGEJA
…………………………………………….
01/02/2014