HOFU kuu iliyopo sasa nchini Afrika Kusini kufuatia kifo cha
aliyekuwa rais wa kwanza mweusi, Nelson Mandela ‘Mzee Madiba’ ni
kupasuka kwa familia yake baada ya mazishi yatakayofanyika kesho
kijijini Qunu, Eastern Cape Mkoa wa Mthatha.

Graca ni mzaliwa wa Msumbiji. Aliwahi kuwa mke wa Rais wa Kwanza wa
Msumbiji, hayati Samora Moses Machel. Pia amewahi kuwa Waziri wa Elimu
wa Msumbiji.
HAKI YA KUMILIKI MALI
Mtandao mmoja nchini humo ulidai kwamba, haki ya kumiliki mali za
marehemu ipo kwa msemaji mkubwa wa familia ya Mandela, Mandla Makgatho
Mandela (39) ambaye ni mjukuu wa kwanza wa marehemu.
Mandla ndiye aliyekabidhiwa mwili wa marehemu na wanajeshi waliobeba
jeneza siku ulipopelekwa kwenye Jengo la Muungano, Pretoria nchini humo.
Mbali na dereva, mtu mwingine aliyekuwa ndani ya gari lililobeba jeneza ni Mandla.
SIFA YA MANDLA
Mandla anatajwa kuwa msemaji mwenye mamlaka ya kufanya lolote
kutokana na wadhifa wake huo ambao hautenguliki kimila. Hata marehemu
alilijua hilo.
MASWALI YA WATU
Maswali mengi ya wakazi wa nchi hiyo ni kama Mandla ataweza
kumchukulia Graca kuwa ni mjane sahihi anayestahili kupata haki sawa.
KUMBUKUMBU
Kabla ya kifo cha Mandela, Mandla aliwahi kuingia matatani na baadhi
ya watoto wa marehemu kufuatia kitendo chake cha kuhamisha miili ya
marehemu wa ukoo huo kutoka Qunu kwenda kuizika upya anakoishi hali
iliyotafsiriwa kuwa, alitaka Mandela akifa akazikwe huko Nvezo.
Ndugu mbalimbali walikuja juu na kumtaka arudishe miili hiyo Qunu la sivyo sheria ingetumika.
“Hatudhani kama Mandla ataweza kumbeba Graca kama mjane sahihi wa
Mandela, wala hatudhani kama familia hiyo itasimama kwa amani baada ya
kifo cha Madiba,” ilisema sehemu ya mtandao huo ikimkariri mmoja wa
raia wa nchi hiyo.
UWEPO WA WINNIE WATIA SHAKA
Habari zaidi zilidai kuwa, uwepo wa Winnie Mandela ambaye aliwahi
kuwa mke wa marehemu kabla ya kutengana baada ya kutoka jela mwaka
1990, ni chachu ya kuweza kuwepo kwa mpasuko huo kwa sababu ana watoto
ambao hawaungi kizazi cha Mandla.
Mandla alizaliwa kwa mke wa kwanza wa Mandela, Evelyn Mase Mandela
hivyo ni rahisi uzao wa Winnie kuwa na msimamo tofauti na msemaji huyo.
NGUVU YA WINNIE NA GRACA
Nchini Afrika Kusini, Graca ametokea kuwa na nguvu zaidi ya Winnie
akichukuliwa kuwa ndiye aliyemtunza mzee Madiba katika kipidni chake
cha uzee, kutoka gerezani hadi kifo.
Winnie, yeye zaidi ya kuwa katika harakati za kupigania uhuru wakati
Mandela akiwa gerezani, alichafuka na skendo yake ya usaliti hivyo
kukosa mvuto kwa jamii ya nchi hiyo.
MANDELA ANAZIKWA KESHO
Merehemu Mandela atazikwa kesho kijijini kwake, Qunu ambako maelfu ya watu wanatarajiwa kuhudhuria.