Yaelekea mwanadada Jackie Cliff alikuwa
amejipanga kisawa sawa na alijitoa muhanga na kujua lolote lingeweza
kumpata kutokana na kazi aliyo kuwa akifanya ya kubeba sembe.
Jackie
alijipanga na kuamua kumuachia rafiki yake kipenzi Martin Kadinda
maagizo na wosia wake just incase ikatokea akafariki. Jackie aliweza
kuandika ujumbe huo kwenye status yake ya BBM kama inavyo onekana hapa
chini.
Jackie alikamtwa mapema mwezi huu Macau, China na kilo 1.1 za heroin na sasa anasubiria hatma yake kutokana na kosa hilo la kusafirisha madawa ya kulevya.