Akithibitisha
tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema
kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo
Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi
hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka
yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
Akizungumza kwa
njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo
alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa
kuusambaza unaomchafua Zitto.
“Kwa kweli sijui
hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni
kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa
tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna
mwingine,” alisema Kileo.