Zitto
pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na
Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada
ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa
ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa
uchaguzi mkuu wa ndani.
Leo,
uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao
pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo
zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto
na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji
wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa
ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Miongoni
mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema
(Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa
makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa
nyadhifa zao.
Mchange
na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana
Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada
ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu
Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM
wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.
Jana,
Machange alipotafutwa, alisema: “Mimi sikuwahi kuondoka Chadema,
nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka
malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema
nimeondoka.
Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.
“Mimi
ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote,
walioondoka ni Mwampamba na Shonza.” Mwampamba alisema: “Nilijitokeza
pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo
nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za
aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama
kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua
dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo
halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu.”
Kuwepo
kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema
kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza
kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu
mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba
wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku
14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini
wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Dk Slaa
Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima
viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika
na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani
ya chama hicho.
“Hata
katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima
ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri.
Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe
kutengenezwa sasa hivi?” alihoji Dk Slaa.
Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa
Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi
mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende
kwa waandishi wa habari?”
“Mimi
ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje
kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji
Dk Slaa.
Mkutano leo
Mkutano
wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu baadhi ya
hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile
alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu
akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.
Habari
zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni
“Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu
hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.
Jana,
Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa
tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani
anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya
hivyo?”
Ofisa
Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu
ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu
kama chama.”
Habari
ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda
uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa
kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni
pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi
ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya
kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu
vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati
Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.
Habari
zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa
ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na
Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila
kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi
ndiyo inapaswa kuiandaa.
Wasomi wanena
Akizungumzia
mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya
Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi.
“Misingi
ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho
nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi
hakuna,” alisema Mbunda.
Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa
Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi
mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: “Wao nani kawaambia waende
kwa waandishi wa habari?”
“Mimi
ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje
kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?” alihoji
Dk Slaa.
Mkutano leo
Mkutano
wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu baadhi ya
hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile
alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu
akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.
Habari
zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni
“Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu”, badala ya kujibu
hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.
Jana,
Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa
tuhuma za kusema na za kuacha... “Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani
anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya
hivyo?”
Ofisa
Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: “Kamati Kuu
ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu
kama chama.”
Habari
ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda
uongozi wa Chadema ukaweka wazi “makosa mengine” ambayo Zitto anadaiwa
kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni
pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi
ya miezi sita. “Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya
kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu
vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati
Kuu imechoka,” alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.
Habari
zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa
ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na
Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila
kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi
ndiyo inapaswa kuiandaa.
Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani
ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala
hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani.
Mhadhiri
Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk
Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu
wenye malengo na mitazamo tofauti.
“Ukisoma
huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye
uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke
kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa
walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi,” alisema. Alisema haoni kwa nini
Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo
walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi.
“Mabadiliko
ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao
inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi
wakiwafukuza uanachama,” alisema Makulilo.