Kazi
ya kwanza nilifanya Bungeni ilikuwa ni kuhesabu kura za kumthibitisha
Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa. Spika Samwel Sitta aliteua mbunge
mwenye umri mdogo zaidi na mbunge wa kuchaguliwa mwenye umri zaidi.
Amina Chifupa na mie tulienda kuhesabu kura zile. Kura 3 ziliharibika.
Karani wa Bunge akatuomba tusirekodi kura zilizoharibika kwani ni aibu
kwa wabunge. Amina akakataa kwa kusema "aibu gani, wananchi wawajue
wabunge wao"! Nilishikwa butwaa. Wakati huo watu wengi walimdharau
mbunge huyu kama 'mtangazaji' tu tena wa mipasho. Jioni ya siku ile
Disemba 29, 2005 ilibadili kabisa mtazamo wangu kuhusu watu na uwezo
wao. Amina alishangaza wengi kiuwezo hasa vita yake dhidi ya dawa za
kulevya.