
Basil Mramba.
Mawaziri hao ni Basil Mramba na Daniel Yona na katibu Grey Mgonja, ambao kesi yao iko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wanatuhumiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuisamehe kodi, Kampuni ya Ukaguzi wa Madini ya Alex Stewart, kinyume cha sheria.
Hayo
yalibanishwa jana na Hakimu Mkazi Alphan Isaya, wakati akiahirisha
kesi hiyo.Jana ilikuwa siku ya kuendelea kusikiliza utetezi wa
washtakiwa hao, lakini mshtakiwa Yona hakuwepo mahakamani.
Awali, Wakili wa Serikali, Oswald Tibabyekomya, alisema kesi hiyo ilipangwa kuendelea kusikilizwa.
Hata
hivyo Wakili wa utetezi, Eliasa Msuya, aliieleza mahakama kuwa Yona
hakuwepo mahakamani na kwamba yuko India, kwa matibabu na kwamba ana
kibali cha mahakama, kilichotolewa Oktoba 8 mwaka huu.
Kutokana
na maelezo hayo ya wakili wa utetezi, Wakili wa Serikali,
Tibabyekomya, aliiomba mahakama, upande wa utetezi ueleze ni lini
atakuwepo.
MWANANCHI
MWANANCHI