RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kutangaza majina ya mawaziri watano
mapema wiki hii,taarifa za ndani kutoka Ikulu ya Rais Kikwete iliyonaswa
na Habarimpya.com zinaeleza kwamba, zoezi hilo limepangwa kufanyika
mapema wiki hii kabla ya Rais kuanza zoezi la kuteuwa wabuge wa bunge la
Katiba.
"Rais anamajukumu mengi sana ya kitaifa kipindi hiki na moja ya majukumu
yake ni kufanya uteuzi wa mawaziri watano watakaojaza nafasi zilizo
achwa wazi kabla ya Bunge la Katiba kuanza"kilisema chanzo cha
Habarimpya.com kutoka Ikulu ya Rais Kikwete Magogoni jijini Dar es
Salaam.
Chanzo hicho pia kilifafanua kwamba baadhi ya majina yanayotajwa kuingia
katika wizara hizo ni pamoja na Mbunge wa kuteuliwa Dk Asha-Rose Migiro
(Wizara ya Fedha na Uchumi),James Lembeli (Wizara Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa).
Wengine ni Lazaro Nyalandu na Naibu wake kuwa Dk Mary Mwanjelwa (Wizara
ya Maliasili na Utali),January Makamba (Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi) huku nafasi yake ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia, ikichukuliwa na Vita Kawawa (Mbunge wa Namtumbo),Jenista
Muhagama (Wizara ya Mifugo na Uvuvi).
Kuhusu nafasi za Manaibu Waziri katika Wizara hizo, Chanzo chetu
kilidokeza kwamba kuna uwezekano wa manaibu waliokuwepo katika Wizara
hizo kuendelea katika nafasi zao, ingawa orodha hiyo inaweza kubadilika
wakati wowote.
"Mpaka hivi sasa hayo ndiyo najina ninayofahamu kwamba yako mezani kwa
mzee,kutokana na jinsi ambavyo yanatajwa mara kwa mara,ingawa lolote
linaweza kubadilika, kwani kazi ya kuteuwa mawaziri inahitaji umakini wa
hali ya juu, hivyo usije ukashangaa kuona mabadiliko katika orodha
hiyo"chanzo hicho kilifafanua.
CHANZO; PAPARAZI
CHANZO; PAPARAZI
