Okwi alitua nchini juzi Alhamisi tayari kuitumikia
klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani baada ya kutokea sintofahamu
kuhusu uhamisho wake wa kutoka SC Villa kuja Yanga.
Si bajaji, pikipiki achilia mbali magari
yaliyofurika kwenye uwanja huo huku Okwi mwenyewe akisema, “Nimefurahi
sana na mapokezi niliyopewa na viongozi na mashabiki wa Yanga,
nitafurahi kama nitacheza mechi ya kesho,” alisema Okwi ambaye janUwanja wa Bora uliopo Kijitonyama jana ‘ulifurika’ mashabiki wa Yanga waliokuwa na shauku ya kumwona mshambuliaji wao mpya Emmanuel Okwi akifanya mazoezi na timu hiyo.

nitafurahi kama nitacheza mechi ya kesho,” alisema Okwi ambaye jana
alifanya mazoezi kwa mara ya kwanza na Yanga.
Akisisitiza umuhimu wa yeye kucheza alisema,
“Mrisho Ngassa nimecheza naye Simba, Hamis Kiiza tunacheza naye timu ya
taifa (Uganda), hakuna wasiwasi, mimi nikipangwa nao tutacheza kwa
uelewano sana pale mbele na nitafunga.”
Alisema kwa jumla anaijua Yanga vizuri na anajua
uchezaji wa wachezaji wake wengi, hivyo anaweza kucheza vizuri katika
mfumo wa timu hiyo.
“Unaweza kuitwa timu ya taifa, siku mbili kabla ya
mechi na wakati mwingine unakuta wachezaji wengi hujawahi kucheza nao
kabisa, lakini mnafanya mazoezi siku moja mnaelewana na mnacheza
vizuri,” alisema Okwi.
Kwa upande wa kocha wa timu hiyo Ernie Brandts
alisema Okwi ni mwepesi na anakasi na anajua kutengeneza nafasi za
kufunga mabao na atampanga katika mchezo wa leo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya mahasimu wao.
Jezi za Yanga zenye jina la Okwi zimetapakaa na
zimekuwa zikigombewa kama njugu na mashabiki wa klabu hiyo ambayo mara
zote walisikika wakiimba Okwi... Okwi...
Na kabla ya kuanza mazoezi, Brandts alimtambulisha, Okwi kwa wachezaji wenzake na benchi la ufundi.
a