LOWASSA AWAAMBIA BODABODA: NUNUENI PIKIPIKI, MSIWATAJIRISHE WENGINE


Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Wilaya ya Ilala, Michael Loswe (kushoto), akisoma risala kwa mgeni rasmi, Edward Lowassa.

Kamanda wa Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (kushoto), akiteta jambo na Lowassa.…
Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Wilaya ya Ilala, Michael Loswe (kushoto), akisoma risala kwa mgeni rasmi, Edward Lowassa.
Kamanda wa Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga (kushoto), akiteta jambo na Lowassa.
Michael Loswe akikabidhi risala kwa mgeni rasmi, Mhe. Lowassa.
Mgeni rasmi, Edward Lowassa akiongea na waendesha bodaboda (hawapo pichani).
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, akiongea na waendesha bodaboda (hawapo pichani).
Mmoja wa waendesha bodaboda akiruka kumshangilia Lowassa.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Linex, akiwa amebebwa na waendesha bodaboda kumpeleka jukwaani.
Linex akitoa burudani. Umati wa waendesha bodaboda wakimshangilia Linex.
Bodaboda zikiwa zimepaki eneo la hafla hiyo.
Lowassa akiwapa dole waendesha bodaboda.
Ney wa Mitego akitoa burudani.
Waendesha bodaboda wakisukuma gari la Lowassa.
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowasa, leo asubuhi amewataka waendesha pikipiki (bodaboda) wa wilaya zote za  jijini Dar es Salaam ambazo ni Ilala, Temeke na Kinondoni kununua pikipiki zao badala ya kuendelea kutumia pikipiki zinazowatajirisha watu wengine ambao wanazimiliki.
Lowasa ambaye ni Mbunge wa Monduli aliwataka waendesha bodaboda hao kuanzisha vyama vya kuweka na kukopa (Saccos)  ambazo zitawasaidia kujiongezea kipato na kujinunulia pikipiki zao na kuachana na kuendesha pikipiki za matajiri.