
“Mimi nipo baridi, nasubiri kwa hamu kubwa kuitwa kwenye Kamati Kuu,
mimi si mtu wa kupiga kelele na tuhuma zote dhidi yangu ninaamini si za
kweli... wakati mwingine maadui wanatafuta njia za kunichonganisha na
chama changu.”
Dk Shukuru Kawambwa
Bagamoyo. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amejibu madai yaliyotolewa hivi karibuni na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kwamba ni mmoja wa mawaziri walioshindwa kazi, hivyo kustahili kung’olewa.
Katika
madai yake, Nape alisema Dk Kawambwa ameshindwa kusimamia vyema madai
ya walimu na kwamba akiwa Waziri wa Miundombinu, aliingia mkataba na
Kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya kujenga Barabara
ya Namtumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana uwezo wa kuijenga.
Nape
alikaririwa akisema kwamba umefika wakati kwa waziri huyo na wenzake wa
Fedha, Dk William Mgimwa; Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher
Chiza; na Naibu wake, Adam Malima kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya chama
hicho.
Akijibu
madai hayo Mjini Bagamoyo jana, Dk Kawambwa alisema anasubiri kwa hamu
kuitwa CC kueleza tuhuma zinazomkabili huku akijigamba kuwa yeye ni mti
wenye matunda ndiyo maana unapigwa mawe.
Alisema
hayo alipokuwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu 16 zitakazoshiriki
michuano ya Kombe la Kawambwa inayofanyika katika Jimbo la Bagamoyo
ambalo yeye ni mbunge wake.
“Kuna
maneno yanayoendelea hivi sasa eti na mimi mbunge wenu natajwa kuwa
fisadi kwa mkataba wa ukandarasi wa barabara, siyo kweli. Wakati
mkataba ule unasainiwa mimi nilishatoka kwenye Wizara ya Miundombinu,
sihusiki kabisa na mkataba ule,” alisema na kuongeza:
“Mwaka
2010 mimi ndiye niliyeshawishi Ubalozi wa Japan ukatoa fedha kwa ajili
ya mradi ule wa Barabara ya Namtumbo - Tunduru lakini mkataba
ukasainiwa Desemba 24, 2012 kati ya Wizara na Kampuni ya Progressive.
“Walipovurunda
Wizara ikawatimua, mimi sikuhusika hata kidogo kwani wakati wanasaini
mkataba ule mimi nilishahamishiwa wizara nyingine.”
“Mimi
nipo baridi, nasubiri kwa hamu kubwa kuitwa kwenye Kamati Kuu, mimi si
mtu wa kupiga kelele na tuhuma zote dhidi yangu ninaamini si za
kweli... wakati mwingine maadui wanatafuta njia za kunichonganisha na
chama changu.”
“Wanasema
kila wizara ninayopelekwa ninavurunda, nasema, mimi ni mti wenye
matunda. Mti wowote ambao unazaa vizuri lazima utapigwa mawe, nasubiri
siku hiyo ya kuitwa CC ambako pumba na mchele vitajulikana.”
Akizungumzia
ujenzi wa barabara hiyo, Waziri Kawambwa alisema anamshukuru Waziri wa
Ujenzi, Dk John Magufuli aliyemfukuza mkandarasi huyo Progressive kwa
kushindwa kazi. Hata hivyo, katika madai yake, Nape alisema kumfukuza
mkandarasi huyo pekee hakutoshi, bali aliyehusika kumpa mkataba naye
anapaswa kuchukuliwa hatua kwani uchunguzi unaonyesha kuwa
alishashindwa kazi wakati anapewa mkataba.
Hata
hivyo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikaririwa na Gazeti
la The Citizen akisema kuwa Chama Cha Mapinduzi hakina mamlaka ya
kuingilia utendaji wa Serikali kwani kinatakiwa kuishia katika ngazi za
watendaji wa cha
MWANANCHI
Kinana
Wakati
huohuo, Lauden Mwambona anaripoti kutoka Tukuyu, Mbeya kwamba, Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewalaumu viongozi wa chama hicho
ngazi za mikoa na wilaya kwa kushindwa kuisimamia Serikali na
kusababisha Watanzania wengi wakupoteza imani nacho.
Kinana
alisema hayo jana alipokuwa akihutubia wakazi wa Halmashauri ya
Busokelo wilayani Rungwe katika Mji mdogo wa Kandete katika siku ya
pili ya ziara yake mkoani Mbeya.
Alisema
Serikali Kuu inapeleka fedha nyingi kwenye halmashauri na mikoa lakini
matokeo yake zinaishia kwenye matumbo ya watu jambo ambalo
limewakasirisha Watanzania wengi.
Aliwataka
viongozi wa CCM kufuatilia fedha zinazoingia kwenye miradi ya maendeleo
na kama Serikali haikutuma fedha hizo, ipo haja ya CCM kufuatilia kwa
viongozi wakuu wa nchi.
Kuhusu
uchaguzi ndani ya CCM, aliwasihi viongozi hao kuachana na tabia ya
kuwapendelea watu wanaotoka mijini au nje ya eneo husika wanaotaka
kuwania uongozi badala ya kuwasikiliza kwanza wagombea wanaotokana na
wananchi wenyewe.
“Tuachane
na tabia ya kuwateua vigogo wenzetu au wenye fedha kugombea nafasi za
uongozi ndani ya CCM au Serikali. Tuwasikilize wananchi wanamtaka
nani,’’ alisema.
Leo Kinana anatarajia kuendelea kuwahutubia wananchi wa vijiji vya Masoko na Ikuti.
ma.MWANANCHI