UKAWA wapata Pigo Jingine mkoani Simiyu....Wananchi wawapokea kwa Mabango ya kuwataka warudi bungenii kujadili matatizo yao na si muundo wa Serikali


Umoja  wa  katiba  ya  wananchi ( UKAWA ) , juzi  wamepokelewa  kwa  mabango  katika  wilaya  ya  Bariadi, mkoani  Simiyu  yaliyowataka  warudi  bungeni  kabla  ya  kuanza  mkutano  wao  kwenye  uwanja  wa  michezo  wa   Halmashauri  ya  mji  huo  ambao  ulihudhuriwa  na  watu  wachache.....

Mabango  hayo  yalikuwa  na  ujumbe  uliowataka  wajumbe  wa  umoja  huo  kurudi  bungeni  kujadili  rasimu  ya  pili  ya  katiba  ili  kushindana  kwa  hoja  na  wajumbe  wa  bunge  hilo  weye  mtazamo  tofauti  na  wao....

Ujumbe  wa  Umoja  huo  ulioongozwa  na  mwenyekiti  wa  vijana  chama  cha  demokrasia  na  maendeleo  ( BAVICHA ) taifa, Bw. John Heche  ulishangaa  kuona  mabango  hayo  na  mahudhurio  ambayo  hawakuyatarajia  licha  ya  mkutano  huo  kutangazwa  siku  mbili  katika  mji  mzima....

Wakiwa  wamebeba  mabango  hayo, wananchi  hao  waliutaka  ujumbe  huo  kuwashawishi  wajumbe  waliosusia  vikao  vya  bunge  warudi  bungeni  ili  kujadili  matatizo  ya  watanzania  na  si  muundo  wa  serikali....

"Sisi  hatuna  haja    na    muundo  wa  serikali  hata  zikiwa  10 , mbili  au  3, tunataka  kunufaika  na  pamba,bei  iongezeke, tupate  pembejeo  za  kutosha  na  kupewa  matrekta  ili  tuweze  kunufaika," alisema  Bw. Mugata Munghu.

Wakazi  wengine  walioshiriki  mkutano  huo  walidai  asilimia  kubwa  ya  wakazi  wa  mkoa  huo  ni  wakulima  na  wafugaji  ambapo  changamoto  kubwa  waliyo  nayo  ni  ukosefu  wa  maeneo  ya  kufanyia  uzalishaji....

"Hatuna  maeneo ya  kulishia  mifugo  yetu  na  kufanya  shughuli  za  kilimo,rudini  bungeni  mkatutetee  tupate  maeneo  ya  kutosha  kwa  ajili  ya  wafugaji  na  wakulima, tunataka  kuachana  na  mapigano  ya  kila  siku, wekeni  sheria  ya  kuilazimisha  serikali  itenge  maeneo  haya, hatuoni  umuhimu  wa  nyie  kutanga taga  nchi  nzima  kutaka  serikali  tatu," alisema  Bw. John Matale

Viongozi  wa  umoja  huo  waliendelea  kuhutubia  mkutano  huo  mbali  ya  kuwepo  kelele  za  vijana  waliokuwa  wakizunguka  na  mabango  huku  viongozi  hao  wa UKAWA  wakitumia  muda  mwingi  kumshambulia  katibu  mkuu  wa  CCM,Abdulrahman  Kinana.
  
                          ....MPEKUZI

KESHO NITAWAAMBIENI UKWELI KUHUSU TUKIO HILI AMBALO MPEKUZI ANAJARIBU KUDANGANYA WATANZANIA

AJALI MBAYA YATOKEA... YAUA WENGI NA WENG MAJERUHI




WATU watano wamekufa papo hapo na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya barabarani iliyolihusisha gari dogo la abiria aina ya Toyota Hiace eneo la Mlima Sekenke, wilayani Iramba kwenye Barabara Kuu ya Singida -Mwanza.
 
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba, Dk Antony Mbulu, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:30 usiku wakati abiria hao wakienda kwenye sherehe ya Maulid kijiji jirani cha Shelui.
 
Dk Mbulu aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni dereva Athuman Adam (34) na Ally Wambura (36), wakazi wa Igunga na Amin Salim (45) mkazi wa mjini Singida. Alisema miili ya watu wawili haijatambuliwa.
 
Kwa mujibu wa Dk Mbulu, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi hilo lenye namba za usajili T547 ASP kushindwa kulimudu kutokana na mwendo kasi.
 
Alisema kuwa majeruhi watano kati ya 16 waliolazwa kwenye hospitali hiyo, wamehamishiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida kwa matibabu zaidi huku hali zao zikielezwa kuwa mbaya.
 
Baadhi ya majeruhi ambao hawakutaka kutajwa majina yao, walisema ajali hiyo ilitokana na mwendo kasi na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
 
Walidai kuwa ajali ilitokea wakati dereva huyo akipita malori kwa kasi, ndipo akagonga kingo za barabara na kupasua tairi kabla ya kuingia msituni na kupinduka mara nne.
 
Basi hilo dogo lilikuwa limebeba abiria 21 likitoka mjini Singida kwenda Shelui.

Majani ya Mapapai hayatibu Dengue....Wananchi washauriwa kutokubali kudanganywa na waganga wa jadi




Halmashauri  ya  manispaa  ya  Ilala  imesema  kuwa  majani  ya  mapapai  si  tiba  ya  ugonjwa  wa  dengue  hivyo  ni vyema  wananchi wakafika  hospitalini  kupatiwa  dawa  kuliko  kudanganywa  na  waganga  wa  jadi....


Kauli  hiyo  ilitolewa  Dar es Salaam jana  na  kaimu  mganga  mkuu  wa  manispaa  ya  Ilala, Dr  Willy Sango, wakati  wakitoa  mafunzo  kwa  wenyeviti  wa  serikali  za  mitaa  jinsi  ya  kuelimisha  wananchi  jinsi  ya  kujikinga  na  homa  ya  dengue...

Dr Sango  alisema  ugonjwa  wa  dengue  hauna  tiba  wala  chanjo  bali  wanatibu  dalili  za  ugonjwa  huo  tu, hivyo  ni  vyema  wananchi  wakachukua  tahadhari  ya  kujikinga  nao....

Pia  aliwataka  waganga  wa  jadi kuacha  kuwadanganya  wananchi  kwa  kusema  kuwa  majani  ya  papai  yanatibu  kwani hiyo  si  kweli  na  hayajathibitishwa  na  wataalam  wa  afya...

Alisema  kuwa  mtu  akiugua  anatakiwa  aende  hospitali  kwanza, asiende  kutumia  dawa  bila  kupima  kwani  hiyo  ni  hatari, hivyo  wananchi  wanatakiwa  kufika  hospitalini  kupima  ndipo  waanze  kutumia  dawa....

Hata  hivyo  alisema, wenyeviti  wa  serikali  za mitaa  wanatakiwa  kuhakikisha  wanasimamia  vizuri  maeneo  yao  pamoja  na  kushauri  wananchi  kwenda  hospitali  na  kuacha  kudanganywa  na  majani  ya  mapapai....

"Majani  ya  papai  si  dawa  ya  dengue  wala  hayajathibitishwa  na  mpaka  sasa  hakuna  dawa  ya  ugonjwa  huo. Tunacho tibu  ni  dalili  zake  tu, hivyo  wananchi  msidanganyike  na  waganga  wachache  wanaotaka  pesa," alisema  Dr  Sango

Pia  alisema  kuanzia  kesho, dawa  zitaanza  kupuliziwa  mtaa  mmoja  baada  ya  mwingine  ili  kuua  mazalia  ya  mbu  hao  wanaoeneza  ugonjwa  huo....

Hata  hivyo  alisema  kuwa  watu  wanaopulizia  dawa  hizo  wanatakiwa  kufika  katika  ofisi  za  serikali  za  mitaa  ili  watambuliwe  kwanza  ndipo  waendelee  na  zoezi  hilo.

Walimu washauriwa kuacha kutumia VIROBA wakati wa kufundisha

Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari Tanzania kanda ya mashariki kupitia umoja wao TAHOSSA wakimsikiliza ofisa elimu mkoa wa pwani hayupo alipofungua mkutano wao mjini Kibaha.
Picha ya pamoja na baadhi ya walimu wakuu wanaounda umoja wao wa TAHOSSA Kanda ya mashariki.

Na John Gagarini, Kibaha
OFISA Elimu Mkoa wa Pwani Yusufu Kipengele amewataka walimu mkoani humo kuachana na tabia ya kutumia vilevi waingiapo madarasani kufundisha kwani hali hiyo inachangia kushuka kwa kiwango cha elimu.
 
Imebainika kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia vilevi aina ya viroba kabla ya kuingia madarasani kufundisha hali ambayo ni moja ya sababu ya kiwango cha elimu kushuka ambapo mwalimu husika kufundisha chini ya kiwango.

Aliyasema hayo juzi mjini Kibaha wakati akifungua kikao cha umoja wa walimu wakuu wa shule za sekondari Tanzania (TAHOSSA) kanda ya Mashariki na kusema kuwa tabia kama hiyo haipaswi kufumbiwa macho na viongozi wa idara ya elimu ili kurekebisha mwenendo wa walimu.

“Baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia pombe aina ya viroba jambo ambalo limekuwa likichangia maadili kuvunjika kwa walimu na wanafunzi wanaowafundisha,” alisema Kipengele.
 
Alisema kuwa baadhi ya walimu wamekuwa wakitumia vilevi hivyo pamoja na wanafunzi hivyo kufanya taaluma kushuka kwani walimu hao uwezo wao unashuka na kushindwa kuwapatia kile wanachotakiwa kuwafundisha wanafunzi.

Akijibu baadhi ya hoja ikiwemo ya kukosa fedha kwa ajili ya wasimamizi wa mitihani ya vitendo aliwataka kuhakikisha wanapeleka suala hilo kwenye uongozi wa bodi ili waridhie ili wazazi wachangie sehemu ya gharama hizo ambapo kwa upande wa serikali nayo itachangia kwa kiasi.

Awali akimkraibisha mgeni rasmi ambaye ni ofisa elimu wa mkoa mwenyekiti wa TAHOSSA Omary Msami alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubw aikiwa ni pamoja na mitihani ya vitendo kutokuwa na fedha toka wizarani.

“Tunaomba tupatiwe mafunzo kazini kwani walimu hawapatiwi jambo ambalo linasababisha walimu kushindwa kwenda na wakati kwani baadhi ya mambo ya ufundishaji yamekuwa yakibadilika,” alisema Msami.

Aidha aliomba ukaguzi mashuleni ufanywe kila mwaka ama baada ya miaka miwili ili kurekebisha kasoro zinazojitokeza na kuwalipia wakaguzi hao ili kuzipunguzia mizigo shule.
 
Umoja huo unaundwa na mikoa ya Pwani na Morogoro ambapo kuna jumla ya shule 384 na walimu wakuu 131.

UKAWA WAFUNIKA IRINGA, CHEKI TUKIO ZIMA LILIVYOKUWA




UMOJA  wa  Katiba  ya  Wananchi  (  UKAWA )   umepokelwa  kwa  mabango  yanayowapinga  wilaya  ya  Mufindi  mkoani  Iringa  yaliyokuwa  yamebebwa  na  vijana....


Mabango  hayo  yalikuwa  yanasomeka  kuwa, "Tuna  mashaka  na  ndoa  ya  UKAWA  watauza  nchi", huku  yakisisitiza  umuhimu  wa  vijana  wa  Wilaya  ya  Mufindi  kutaka  Serikali  mbili.....

Pia  mabango  hayo  yalikuwa  yanawataka  wajumbe  wa  UKAWA  warudishe  posho  kwanza  bungeni  mjini  Dodoma....

Katika  mkutano wao   uliofanyika  juzi mjini  Mafinga  Viwanja  vya  mashujaa, mkutano  huo  uliendeshwa  na  mwenyekiti  wa  chama  cha  Wananchi ( CUF )  ambaye  pia  ni  mwenyekiti  mwenza  wa  UKAWA.....

Wengine  waliohutubia  ni  pamoja  na  mwakilishi  wa  chama  cha  NNCR-Mageuzi,Danda  Juju  na  kiongozi wa  taasisi  ya  kiislam  ya  Shura  ya  Imamu,Rajabu  Katimba.....

Baadhi  ya  mabango  yaliyokuwa  yamebebwa  na  vijana  hao  wilayani  Mufindi  yalikuwa  na  ujumbe  uliosomeka: "Vijana  Mafinga  tuna  mashaka  na  ndoa  ya  UKAWA,watauza  nchi" na  bango  la  waendesha  bodaboda  lilisomeka: "Rudisheni  posho  kwanza  mjengoni  Dodoma"

Mengine  na  ujumbe  wake  kwenye  mabano  ni lililowatambulisha  wafanyabiashara  wa  sokoni  lililosomeka, "Mafinga  Sokoni,Serikali  tatu  siyo  suluhisho  la  matatizo  ya  wananchi", na  la wapiga  debe  mafinga  stendi  lilisomeka, "Karume  Oyee, Nyerere Oyee, Muungano  Saafi!".

Bango  la  waliojitambulisha  kuwa  ni  machinga  lilisomeka, "Tunataka  Serikali  inayojali  wajasiriamali, siyo  kujali  matumbo  yao"...Na  lile  la  wakulima  lilisomeka, "Kilimo  Kwanza, Utaifa  kwanza".

Wakati  mabango  hayo  yakizungushwa  katika  mkutano huo  muda  ambao  Profesa  Lipumba  alikuwa  akihutubia, usikivu  ulipotea  kwa  takribani  dakika  15  hadi  20  baada  ya  sehemu  ya  kundi  la  vijana  lililokuwa  likimsikiliza  kuelekea  upande  walikokuwa  vijana  wenye  mabango  hayo....

Polisi  waliokuwepo  walilazimika  kuingilia  kati  kadhia  hiyo  na  mzozo  huo  baina  yao  na  vijana  waliokuwa  na  mabango  ulisikika....

Mmoja  wa  polisi  aliyekuwa  akiwatuliza  vjana  hao  alisema,"Jamani  huu  ni  mkutano  halali  wa  kisiasa, acheni  wenzenu  wafanye  mkutano  wao, yatoeni  mabango  yenu"

Mmoja  wa  vijana  aliyekuwa  amebeba  bango  mojawapo  jina  halikupatikana  mara moja  alisikika  akisema, "UKAWA  siyo  chama  cha  siasa, wao  wanamtazamo  wao  na  sisi  tuna mtazamo  wetu, kwa  hiyo  siyo  jambo  la  ajabu  wakajua  kwamba Mafinga  wengi  hatuwaungi  mkono  na  siyo  dhambi  kuonyesha  hisia  zetu  katika  mkutano  wao"

Akielezea  vurugu hizo, profesa  Lipumba  alisema zinafanywa  na  vijana  waliotumwa  na  CCM  kwa  sababu  ya  msimamo  wao wa kutaka  serikali mbili, tuhuma  zilizokanushwa  na  katibu  wa  CCM wilaya  ya  Mufindi,Miraji  Mtaturu  aliyehojiwa  baada  ya  mkutano  huo...

"Siamini  kama  mkutano  huu  ungekuwa  unahutubiwa  na   mwenyekiti  wa  CCM wa taifa  Jakaya  Kikwete  wangekuja  na  mabango  yao  na  kufanya  vurugu  hizi," alisema  Lipumba  na  sauti  toka  kwa  baadhi  ya  vijana  hao  zikasikika  zikisema, "Kama  angekuja  na  msimamo  wa  serikali  tatu  ni lazima  angekutana  na  mabango  haya, sisi  tunataka  serikali  mbili"

Hata  baada  ya  vurugu  hizo  kutulia  na  Profesa  Lipumba kuruhusu  maswali  baada  ya  kufafanua  sababu  mbalimbali  zilizowafanya  wasusie  bunge  la  katiba  na  kuanzisha  UKAWA, mkutano  huo  ulitaka  kuvurugika  tena....

Swali  liliotaka  kuuvuruga  mkutano  huo  lilitoka  kwa  kijana  aliyejitambulisha  kwa  jina  la  Rahid  Rashid  ambaye  alitaka  kujua  kwa  nini  CCM  hawapo  katika  umoja  huo.

Pamoja  na  vijana  wengine  kupiga  kelele  wakiashiria  kuwa  hilo  siyo  swali,Profesa  Lipumba  alijibu  na  kusema  hilo  ni  swali  zuri.

Alisema  milango  ya  UKAWA  ipo  wazi  kwa  mtu  yeyote  ndani  na  nje  ya  bunge  la  katiba  wakiwemo  wabunge  na viongozi  wa  CCM

"Tutafurahi  kuwapata  wana  CCM,tunawakaribisha  UKAWA  ili  kwa  pamoja  tushirikiane  kupata  katiba  inayotokana na  wananchi," alisema

Mwingine  aliyeuliza  swali  alikuwa  Winfrida  Ngoti  aliyesema  harakati  za  kudai  serikali  tatu  hazitakuwa  na  maana  yoyote  kama  matatizo  ya  wananchi  hayatashughulikiwa.

"Watanzania  wana  matatizo  lukuki,vituo  vya  huduma  za  afya  havina  wataalamu,dada,wakulima  hawapati  pembejeo  kwa  wakati  na  bei  zake  ni  kubwa, wafanyabiashara  wadogo  wanabanwa  na  kukamuliwa  kodi, walimu  haapati  mishahara  kwa  wakati, askari  wana mishahara  midogo ," alifafanua

Katika  majibu  yake, profesa  Lipumba  alisema  hayo  yote  yatafanyiwa  kazi  kukiwa  na  katiba  bora  itakayosisitiza  uwajibikaji  na  uadilifu.

Polisi Yanasa mtandao wa watu wanaosafirisha wasichana Toka Tanzania na kuwapeleka China kwa ajili ya Kuwatumikisha Kingono




BAADA ya kuwepo malalamiko ya wasichana wadogo wa nchini kusafirishwa kwenda China kutumikishwa katika biashara ya ngono pamoja na dawa za kulevya, sasa serikali imenasa mtandao huo.

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe alitoa taarifa hiyo juzi bungeni wakati akihitimisha michango kuhusu bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2014/15 iliyopitishwa.
 
Chikawe ambaye hata hivyo hakufafanua kwa undani wa mtandao huo ulivyokamatwa, alieleza Bunge namna watoto hao wanavyopatikana kabla ya kufikishwa nchi hiyo ya nje.
 
Kwa mujibu wa Waziri, watu hao wamekuwa wakichukua watoto wadogo na kuwaambia kwamba wanawapeleka China hususani mji wa Guanzhou kuwaajiri kwenye saluni na maduka.
 
Alisema kinara wa usafirishaji amekuwa akitambuliwa kwa jina la ‘Mama’ ambaye baada ya kufika nchini humo, huwanyang’anya watoto hao hati zao za kusafiria. Imebainika zipo hata wakala zinazojihusisha na biashara hiyo haramu ya binadamu.
 
“Wakifika, Mama anawanyang’anya pasipoti zao. Anawaambia ili kuwarudishia, lazima watimize masharti ya kumpa kati ya dola 8,000 na 10,000 baada ya kutumika katika vitendo vya ngono,” alisema Waziri Chikawe.
 
Aliendelea kueleza kuwa wanaposhindwa kutimiza masharti hayo, hukutana na Wanigeria ambao huwapa hati bandia za kusafiria na kisha kuwaingiza katika biashara ya kusafirisha dawa za kulevya kwenda nchi mbalimbali.
 
“Tumenasa mtandao huu…polisi imenasa mtandao,” alisema Waziri na kutoa mfano kwamba hivi karibuni, alikamatwa mtu akiwa na hati ya kusafiria akimpelekea binti mmoja. Alisema binti huyo alipoulizwa juu ya hati hiyo, alikuwa hafahamu anakokwenda.
 
Awali, taarifa juu ya kuwepo usafirishaji wa wasichana wadogo kwenda China kwa ajili ya kutumikishwa katika ngono, ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kutoka ziarani nchini humo.
 
Membe alisema serikali inashirikiana na ubalozi wa China katika kubaini wahusika wa biashara hiyo sanjari na mkakati wa kuhakikisha wasichana hao wanarudishwa nchini.
 
Akielezea mikakati ya serikali katika kukabili biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, Waziri Chikawe alisema katika mwaka wa fedha 2013/2014 Sekretarieti ya kupambana na biashara hiyo imeratibu vikao vinne vya Kamati ya kupambana nayo.
 
Aidha imeandaa kitabu cha anuani na majina ya watoa huduma kwa waathirika wa biashara haramu ya usafirishaji binadamu na vilevile kutengeneza rasimu ya kanuni za sheria ya kupambana na biashara hiyo nchini.
 
Katika mwaka wa fedha 2014/2015 sekretarieti itakamilisha kutengeneza kanuni za Sheria ya kupambana na biashara hiyo ya mwaka 2008. Pia itatoa elimu na kuimarisha mikakati ya kupambana na biashara hiyo ya kusafirisha binadamu.
 
Watanzania zaidi ya 100 wakiwemo wasichana 20 wamedaiwa wapo gerezani nchini China wakijihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mfuko kuboresha makazi ya askari waanzishwa




MFUKO maalumu wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha makazi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwemo askari, umeanzishwa ukilenga kuwezesha kupata nyumba na ofisi zaidi bila kutegemea bajeti ya serikali.

 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe ambaye bajeti ya wizara yake iliidhinishwa juzi, alitoa taarifa hiyo wakati akihitimisha mjadala kuhusu bajeti ya wizara yake.
 
Katika mjadala, wabunge wengi walichangia kutaka maslahi, makazi na ofisi za askari polisi, magereza na uhamiaji yaboreshwe kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi.
 
Bunge liliidhinisha bajeti ya Sh 881,740,291,800 kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2014/2015 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo.
 
Chikawe alisema, “tumeona tusitegemee bajeti ya Hazina (Serikali).” Alisema mfuko ulioanzishwa, ambao bodi yake imeshazinduliwa ikiwa chini ya mfanyabiashara maarufu Ali Mufuruki, unalenga kukusanya fedha kutoka kwa wanajamii kuwezesha kujenga ofisi na nyumba za watumishi na askari wa wizara hiyo.
 
Waziri, ambaye alikiri nyumba za askari katika mikoa mbalimbali kuwa duni na kusema hali hiyo haipendi, alisema mpango huo uliofikiriwa na wizara ni wa uhakika kuliko mipango mingine iliyowahi kubuniwa.
 
Alisema chini ya mpango huo, watahakikisha nyumba chakavu zinaondolewa kwa kujenga mpya.
 
Aliahidi kukaa na waziri kivuli wa wizara hiyo kutoka upinzani, Godbless Lema ili hafla ya uchangiaji chini ya mfuko huo ianzie Arusha kabla ya kwenda kwenye majiji mengine ya Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.
 
Akizungumzia posho ya askari ya Sh 5,000 ambayo wabunge walilalamikia kwamba haitoshi na badala yake iongezwe hadi Sh 7,500, Chikawe alisema wako kwenye majadiliano na Hazina kuwezesha posho hiyo ifike Sh 8,000.
 
Aidha alisema majadiliano mengine yanayoendelea na Hazina, ni ya kuwezesha posho ya chakula ya wafungwa itoke Sh 500 kwa siku hadi Sh 3,000. Chikawe alikiri posho hizo za askari na wafungwa ni ndogo.
 
Alisema kwa wafungwa, wanapokuwa wengi kiasi cha posho hushuka chini ya Sh 500. Tatizo lingine linalokabili wafungwa ni ukosefu wa sare.
 
Alisema hawajamudu kuwezesha kila mfungwa kuingia jela akiwa na sare yake badala yake, husubiri mfungwa anayeondoka kumwachia anayeingia.
 
Hata hivyo, alisema bajeti ya mwaka huu itatosheleza kununua sare. Aidha kwenye maeneo ya baridi, serikali haijamudu kununua nguo nzito za kukabili hali hiyo ya hewa.

>>Habari Leo <

Kijana aliyenunua makahaba wawili na kujifungia nao chumbani kwa lengo la kuwafaidi wote AUMBUKA.....Makahaba wamzidi nguvu,azima na kupoteza fahamu




Mwanaume  mmoja  ambaye  ni  muokota  chupa  maarufu  aliyetambuliwa  kwa  jina  moja  la  Hamad  anadaiwa  kunusurika  kufa  katika  nyumba  moja  ya  kulala  wageni  iliyoko  eneo  la  Manzese  jijini  Dar  kufuatia  kuthubutu  kwake  kufanya  ngono  na  makahaba  wawili  kwa  pamoja.....



Kwa  mujibu  wa  mashuhuda  wa  tukio  hilo, inaelezwa  kwamba  mara  baada  ya  Hamad  kujipatia  pato  lake  baada  ya  kuuza  chupa  za  plastiki,alikwenda  kuwanunua  makahaba  hao  na  kuwataka  wakafanye  ngono  shirikishi.....

"Hawa  makahaba  kazi  yao  ni  kuuza  miili,walipomuona  amekwenda  na  pesa  nzuri  wakamkubalia,kumbe  huyu  bwana  kula  yake  ni  ndogo, mwilini  kwake  kumejaa  gongo  tu  na  wala  hana  chakula  cha  kutosha.Walipokuwa  chumbani  wanawake  hawa  walimzidi  nguvu  akapoteza  fahamu"  Alisema  shuhuda

Aliongeza  kwamba  makahaba  hao  walikuwa  na  utu, baada  ya  kumuona  hajiwezi  walimtoa  chumbani  na  kumpeleka  uwani  ambako  walimmwagia  maji  mpaka  akazinduka....

Hata  hivyo  inaelezwa  kwamba, baada  ya  kurejewa  na  nguvu  kama  kawaida, Hamad  alitaka  tena  kuingia  chumbani  na  warembo  hao  ambao  walimkatalia  na  kutishia  kumtelekeza  akizingua  tena....

Daktari asahau kitambaa tumboni mwa Mgonjwa mkoani Tabora....Mgonjwa atolewa Kizazi na kukatwa sehemu ya Utumbo ili kukitoa kitambaa hicho



Waziri  wa  Afya

MKAZI wa wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Mwamini Adamu ametolewa mfuko wa kizazi na kukatwa sehemu ya utumbo baada ya mganga wa idara ya upasuaji katika wilaya hiyo kusahau kitambaa tumboni kwa mwanamama huyo wakati akijifungua.

 
Kutokana na kumsababishia ulemavu huo kwa uzembe, Mwamini ameifikisha Halmashauri ya wilaya ya Urambo kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Magharibi akidai fidia ya Sh milioni 500.
 
Mwamini ambaye anadai kuwa alipwe kiasi hicho cha fedha kutokana na uzembe wa uliofanywa na Dk Jacob Kamanda aliyemfanyia upasuaji wakati wa kujifungua na kumsababishia aondolewe mfuko wa kizazi pamoja na kukatwa utumbo.
 
Mwamini pamoja na mumewe Idrisa Jafari katika madai yao wametaka walipwe fedha hizo kutokana na makosa ya uzembe uliofanywa na wataalamu wa upasuaji kwa kuacha kitambaa tumboni mwa mama huyo.
 
Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji Amir Mruma jana, mama huyo alidai kuwa Januari 6 mwaka 2011 alijifungua kwa upasuaji baada ya hapo hali yake ilizidi kuwa mbaya huku akitokwa usaha ukeni na sehemu ya tumbo kwenye mshono.
 
Huku akiongozwa na wakili wa kujitegemea Mussa Kwikima, mama huyo aliiambia mahakama kuwa hali hiyo ilifanya apelekwe hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete bila mafanikio ndipo ikamlazimu kwenda Itigi kwa matibabu zaidi.
 
Katika uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa na madaktari bingwa, Haile Sales ambaye ni raia wa Italia pamoja na Anatole Lukonge wa hospitali hiyo ya Itigi, waligundua kuwa kuna kitu tumboni kama uvimbe hivyo wakalazimika kumfanyia upasuaji mwingine.
 
Baada ya upasuaji huo walikuta kitambaa cha rangi ya kijani ambacho kilikuwa kimeozesha mfuko wa uzazi pamoja na utumbo kugandana na kitambaa hicho ikabidi kitambaa hicho kutolewa na kusababisha kupasuka kwa utumbo ili kumnusuru maisha yake.
 
Naye daktari bingwa wa magonjwa ya akinamama na ambaye ni mganga mkuu wa hospitali ya Itigi, Anatory Lukonge katika ushahidi wake ameiambia mahakama hiyo kuwa alimpokea mlalamikaji akiwa anatokwa na usaha ukeni na sehemu iliyoshonwa.
 
Dk Lukonge amebainisha kwamba walipomfanyia upasuaji mama huyo, walikuta utumbo umeshikana na mfuko wa uzazi huku kukiwa na kitambaa kimeng’ang’ania juu yake.
 
Alisema wakati walipojaribu kukiondoa kitambaa hicho kibofu cha mkojo kilipasuka wakalazimika kumuwekea mpira ili uweze kumsaidia kutolea uchafu.
 
Kesi hiyo ya madai namba 13/2011 imeahirishwa hadi Agosti tatu mwaka huu itakapoendelea kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuleta mashahidi wake.

Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere amtokea Mkewe Ndotoni na kumpa UJUMBE mzito kuhusu mwelekeo wa Tanzania.....Bofya hapa kuona alichosema




MKE wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria, amesikitishwa na jinsi baadhi ya watu wanavyomkosoa mwasisi huyo kwa kuwa enzi za uhai wake alifanya kazi kwa bidii katika kulitumikia taifa kiasi cha wakati mwingine kuisahau familia kwa muda.


Akiongea na waandishi nyumbani kwake Msasani, jana, Mama Maria alisema kwa uchungu kuwa mumewe ambaye alifariki miaka 15 iliyopita, amemtokea ndotoni   na kumtaka akalitahadharishe taifa na mwenendo wake.

“Kitendo cha nchi kukumbwa na mashetani wanaovuruga amani na kutukana waasisi kimemfanya Mwalimu Nyerere kunitokea na kunitaka kuliambia taifa kusali na kuomba sana kwani nchi inaelekea katika vitaAlisema jana huku akionesha hisia kali.


Pia, alisema mambo yanayoendelea nchini kwa sasa ni matokeo ya tamaa na kupungua kwa upendo miongoni mwa jamii jambo linalohatarisha usalama na amani ya nchi.

 
Mama Maria alisema ukosoaji wa viongozi waasisi ni tatizo la dunia nzima ambalo limekuwa jinamizi kama ilivyotokea kwenye nchini mbalimbali ikiwemo Misri na Libya, hivyo ili Tanzania iweze kuepukana nalo ni wajibu wa kila mtu kuombea taifa kwa kufikiria tulikotoka na tulipo.
 
Alisema ni wazi kuwa Mwalimu Nyerere alifanya kazi kwa bidii hata kuisahau familia muda mwingine, kwa sababu aliwapenda Watanzania pasipo ubaguzi wowote na kama alikosea mahali ilitokea kwa kuwa na yeye ni binadamu. Hivyo haipaswi watu kumsema tofauti kama wanavyomsema sasa.
 

HUYU NDIYE DC ALIYEWAPANIA VIJANA

Hakika cheo ni dhamana, hivyo ni muhimu kwa wenye dhamana hiyo kujitambua na kuonyesha wanavyoweza kubeba dhamana hiyo kwa jamii husika.
Halima Dendegu, ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Tanga, mkoani Tanga anaweza kuwa mfano wa kuigwa kwa kuonyesha alivyobeba dhamana hiyo ya kuiongoza wilaya kutokana na kugeukia kundi la vijana wilayani kwake akidhamiria kuwakomboa.
Dendegu aliyeteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, Mei mwaka 2012 kuwa mkuu wa wilaya hiyo anaeleza kuwa baada ya kuingia wilayani humo alifanya utafiti na kubaini kundi kubwa la vijana likijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya kwa sababu mbalimbali.
“Nilianza kubaini vijiwe vingi vya vijana na hawana ajira, nilipofuatilia zaidi niligundua wengi wametumbukia katika matumizi ya dawa za kulevya,”anasema Dendegu na kuongeza:
“Nilibaini vijana 867 wavulana na wasichana, walioathirika kwa matumizi ya dawa za kulevya.”
Anabainisha kuwa baada ya kuwahoji vijana hao walitoa sababu mbalimbali za kujiingiza kwenye dawa za kulevya ikiwamo kukosa ajira, makundi na kukata tama.
“Wengine walisema walishawishiwa, wapo waliosema kiingiacho mjini siyo haramu, waliokuwa wakiuza dawa hizo, hata walioshindwa kutimiza malengo yao maishani,” anasema Dendegu.
Anaongeza: “Kwa sababu hiyo, nimeanzisha kituo ili kuwatibu, kimeanza na vijana 150 na 78 kati yao wameanza matibabu wakiwamo wasichana 28.”
Anabainisha kwamba kwa kuwa lengo lake ni kuwaepusha wasirudi kwenye dawa za kulevya katika kituo hicho ameanzisha pia utoaji elimu ya ujasiriamali.
“Tayari tumebabini wenye vipaji mbalimbali, wapo wapenda mpira wa miguu, watengenezaji sabuni hata wasanii wa muziki wa kizazi kipya.”
Anasema kuwa ili kuwajenga zaidi kiafya na kuanikiza vipaji vyao, kila Jumamosi huandaliwa bonanza linaloendana na michezo mbalimbali.
“Pia nimeanzisha michuano ya mpira ‘Dendegu Cup’ litazinduliwa Juni mwaka huu ili kuibua vipaji zaidi, naamini tutatoa vijana wa kucheza timu kubwa,”anasema akidokeza kuwa hata yeye anapenda na kucheza mpira wa pete, volleyball, pia kuimba.

NMB BANK CAREER OPPORTUNITIES,BANK TELLER VACANCIES , MAY 2014


BANK TELLER VACANCIES 



The Organisation
NMB Plc rely on your commitment to achieve its vision and mission of being the preferred Financial Service Partner in Tanzania through innovative distribution, and extensive Branch Network and offering affordable customer focused financial Services to the Tanzanian Community in order to realize sustainable benefits for all Stakeholders.

We are therefore seeking to recruit high caliber, skilled, motivated, result-oriented and self- driven candidates with high integrity to fill the positions of Bank Tellers in Lake Zone (Mwanza, Kagera, Mara and part of Geita regions)

Job Purpose and Summary
Reporting to Branch/Customer Service/Back Office Manager, Bank Teller will be responsible for collecting deposits in the form of cash and cheques and to pay out cash to customers promptly and efficiently.

Specific Duties and Responsibilities will be to:
·         Ensure that daily cash summaries are checked and day’s cash transactions are properly in line with set performance targets.
·         Count cash deposited (accurately) and ensure that it is correctly entered in the computer system or manual ledger.
·         Ensure that cash, withdrawal form or cheques presented are always paid to customers strictly in line with established procedures.
·         Ensure that collected cash calculations are correct, and withdrawal forms and cheques presented are accuracy.
·         Manage the supply of cash by ensuring withdrawing cash from the strong room at the start of the business and ensure that it is deposited back in the strong room at the end of the business.
·         Attend customers’ queries, fast, with confidence whenever asked.
·         Up and cross sell NMB Plc products. 
·         Seek approval from supervisor on payments that exceed his/her specified limit
·         Report any fraudulent behaviour to the supervisor.
·         Ensure that government cheque and other cheques presented by customers to the supervisor for special clearance with BOT or other banks are timely attended.
·         Perform other duties as directed or assigned by his/her superior.

Qualifications, Knowledge and Skills:
·         Must be a holder of University degree/ advanced diploma or diploma (with two years’ experience) in bank related fields from recognize university/college.
  • Computer literate with skills in Word-processing and Spreadsheets.
  • Able to display a high level of attention to details and skills in interviewing clients to assess their integrity.
  • Able to communicate very well in both English and Kiswahili.
  • Creative, innovative and honest
  • Able and willing to work in challenging environments.
  • Able to work under pressure with minimum supervision

Important General Information to interested Applicants:

HOW TO APPLY:

If you are interested please submit the following:
·         A handwritten application letter duly signed, briefly explaining why you are interested in the position
·         CERTIFIED relevant copies of your certificates/testimonials (Final university/college certificate, transcript, Ordinary & Advanced level academic certificates and birth certificate).
·         A detailed CV, showing clearly your competencies and skills, full address at work or at home including telephone /fax, mobile phone and email address.
·         A list of three reliable referees (not relatives) with their full addresses including telephone, fax and mobile phone numbers.

CLOSING DATE:  23rd May, 2014


“NMB PLC IS AN EQUAL OPPORTUNITY EMPLOYER”

Send your application letter to the Zonal Manager, ONLY via specified address hereunder:

     Zone Manager                                         
     NMB Plc Lake Zone,                                           
     P. O. Box 1580,                          
     MWANZA.

SERIKALI YATOA ONYO KWA WANAOTUMA UJUMBE WA NGONO


 Kumtumia mtu ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini Kenya kunaweza kukuweka mashakani.

Maafisa wakuu wanasema kuwa yeyote atakeyepatikana na hatia atafungwa jela kifungo kisichozidi  miezi mitatu .

Afisaa mkuu kutoka tume ya kitaifa ya mawasiliano, Christopher Wambua ameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono pamoja na picha zenye watu walio uchi watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au dola miatano na themanini na nane kama faini au kufungwa jela..
 

Onyo hilo litawaandamana hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya mkononi au kwenye internet.
 

Kwa mujibu wa taarifa za serikali, kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za, smartphone ilipanda hadi asilimia sitini
 - See more at: http://www.paparazihuru.com/2014/05/kenya-watoa-onyo-kwa-wanaotuma-ujumbe.html#sthash.wlBxgoZR.dpuf
Kumtumia mtu ujumbe wenye picha za watu walio uchi na zenye mada ya ngono nchini Kenya kunaweza kukuweka mashakani. Maafisa wakuu wanasema kuwa yeyote atakeyepatikana na hatia atafungwa jela kifungo kisichozidi miezi mitatu . Afisaa mkuu kutoka tume ya kitaifa ya mawasiliano, Christopher Wambua ameambia vyombo vya habari nchini humo kwamba watu wenye tabia hiyo ya kutuma ujumbe wa kingono pamoja na picha zenye watu walio uchi watatozwa hadi shilingi elfu hamsini za Kenya au dola miatano na themanini na nane kama faini au kufungwa jela.. Onyo hilo litawaandamana hasa wale walio na uzoefu wa kutumiana ujumbe kama huo kupitia kwa simu ya mkononi au kwenye internet. Kwa mujibu wa taarifa za serikali, kiwango ambacho watu hutumiana ujumbe wenye mada ya ngono pamoja na picha za watu walio uchi, zao wenyewe au za mtu mwingine kwa simu zao za, smartphone ilipanda hadi asilimia sitini. SOURCE:BBC

ANGALIA PICHA ZA VURUGU ZILIZOTOKEA KWENYE MKUTANO WA UKAWA MOROGORO


Kijana mmoja amepigwakutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge Rose Kamli wakati wa uchaguzi mdogo jimboni Kalenga, mkoani Iringa.


Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Morogoro na baadaye kuokolewa na polisi.
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.
Mmoja wa viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro, lnnocent Zawadi ambaye alikuwepo jimboni Kalenga naye akithibitihsa pia kumtambua kijana huyo.
Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.