“Kikwete
amejitahidi sana tena kwa kiasi chake kuwajibika kwa umma, hii inaoneshwa na
kuwa tiyari kuwapangua mawaziri na manaibu wao wanaokiuka utaratibu wa ufanyaji
kazi kwa Watanzania kwa hili lazima tumpongeze, amekuwa mstari wa mbele
kuwaonesha hao mawaziri wabovu kuwa
utendaji kazi na uwajibikaji vinaenda
sambamba, Kuna watu wakishapewa nyadhifa serikalini bwana wanajifanya miungu
watu, wanawafanya Watanzania kama ngedere. Wanawageuza kuwa chombo cha
kujinyakulia fedha kwa style yoyote ile. Ebu waangalie wale Mawaziri waliokuwa
wanahusika na Operesheni tokomeza they were all feeling comfortable and were
unwilling to take political responsibility, kwa hili busara za Jakaya
zimeonekana” alisema msomi huyo
Lakini what always confuse me ni Uchaguzi
na uteuzi wa Mheshimiwa huyu Mkuu wan nchi, hivi kweli anawashirikisha
wasaidizi wake vizuri au ndio Business as usual, Haiwezekani mawaziri
waeteuliwe mara 2 na wafanye blunder, inabidi tujiliuze kwa nini Kila uteuzi
wake unakuwa wa mashaka mashaka, watu wanaoteliuwa unwaona kabisa ni watu wasio
kuwa na experience yoyote ya Utawala na utendaji kazi katika taasisi kubwa, Ebu
muangalia kama Huyu Philip Mulugo, elimu yake inatatanisha na karirudia kosa
lile lile kwa uteuzi wa Juma Nkamia, Juma Nkamia hana uzoefu wowote wa kikazi
na utawala, kwanza elimu yake ndogo sana hata hiyo degree hana ndio anaitafuta
UDOM kwa sasa, anaenda kuitawala wizara kubwa ambayo ina changamoto nyingi!
Uteuzi wa Dr. Kebwe kuwa naibu waziri wa
Afya ni challenge kubwa kwani hata jimboni kwake hajafanya chochote, jimboni
harudi Wananchi wa pale wanalia kila kukicha sasa hiyo wizara ya madaktari
ataiweza? Ataziweza challenge za akina Ulimboka? Ataziweza Challenge za
madaktari wa Muhimbili?
Unazi wake pia umeonekana kwa kumteua mtoa
mipasho na Naibu katibu wa chama chake bara Mwigulu Nchemba sijui kama huko
Wizarani atapeleka mipasho katika uaandaaji wa
bajeti ya taifa, lazima tuwe tunajiuliza kama Watanzania ni kweli hawa
watu wanatufaa au wamepewa nyadhifa kishikaji na kwa kujuana!
Msomi huyo ameendelea kutudokeza mengi kwa
masharti ya kutotajwa jina na sisi kama kampuni ya Tanzania Kwanza tutafanya
hivo, aliyoyaaongea ni mengi mno mengine yataletwa siku nyingine!