Akizungumza katika "press conference" ya Chadema na waandishi wa habari iliyofanyika leo Mwanasheria mkuu wa Chadema, Mh.Tundu Lisu alisema kuwa mkakati wa kuwachafua viongozi ni wa siku nyingi ambapo Chama kimefanikiwa kunasa mawasiliano ya Zitto tangu mwaka 2009 alipokuwa akiwasiliana akina Denis Msack wa Mwananchi. Lissu alisema njama hizi ndio zilizopelekea mpaka mashtaka ya Ugaidi ambapo katika mahojiano yake ya Star Tv akiwa na akina Mwigulu Nchemba zitto hakukanusha, pia aliandika kwenye mitandao kuwa Chadema imtose Wilfred Lwakatare
Lissu aliongeza kuwa Zitto mpaka sasa ana magari mawili ya Nimrod Mkono
na Mkono mwenyewe ndie amewaambia taarifa hizo. Mkono amewaambia kuwa
amempa Zitto hela nyingi sana na Zitto alishiriki moja kwa moja kumzuia
mgombea wa Chadema katika Jimbo la Nimrod Mkono wakati Nimrod Mkono
alikuwa ni namba sita katika orodha ya Mafisadi iliyotajwa pale
Mwembeyanga.
Lissu alisisitiza kuwa washirika wa usaliti huu na uhaini huu
hawakupenda kutangazwa kuwa wao ni Wasaliti na wahaini lakini yeye
anasema wale ni Wahaini na Wasaliti. Lissu aliasema kuwa Zitto anaendelea kuwa Mwanachama na Mbunge wa CHADEMA kwasababu ya Mahakama tu na sio kwasababu ya mapenzi ya CHADEMA.
Mapema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akitoa maadhimio ya kamati kuu
alisema kuwa Kamati Kuu imeamua kuwavua Uanachama ndugu Samsoni Mwigamba
na Dr. Kitila Mkumbo kuanzia tarehe ya jana baada ya maamuzi ya kikao
cha Kamati Kuu.
Maamuzi hayo ni baada ya kunasa mawasiliano mbalimbali ya Zitto Kabwe na
washirika wake akiwemo anayejulikana kwa jina la Chadema Mpya.
Dr. Slaa anasema malengo ya waraka wa mabadiliko hayakuwa ya kisiasa tu
bali yalikuwa na lengo la kuimaliza chadema na kuwabomoa Viongozi wa
Chama.
Dr. Slaa alisema Kamati Kuu imechukua maamuzi haya kwa uchungu kwasababu
CHADEMA haina lengo la kupunguza wanachama bali kuongeza Wanachama hata
wanaCCM katika kuharikisha ukombozi wa Taifa letu.
Chama kinawatangazia Wanachama wote na wapenzi wote kutokushiriki mikutano ama shughuli zozote za kisiasa zitakazoandaliwa na Zitto Kabwe na Washirika wake kwa jina la Chama
