Airtel yazawadia washindi Sh130 mil
Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (kushoto)
akizungumza kwenye simu na mmoja wa washindi wa droo ya wiki ya
promosheni ya Mimi Bingwa. Kulia ni Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi ya Mchezo
wa Kubahatisha Tanzania, Chiku Saleh.
Promosheni ya Mimi ni Bingwa iliyoanza mwishoni
mwa Novemba mwaka jana, inalenga kurudisha sehemu ya pato la kampuni kwa
jamii inayoizunguka.
imeshuhudia wateja 82 wakiibuka washindi katika droo za kila siku na kila wiki.
imeshuhudia wateja 82 wakiibuka washindi katika droo za kila siku na kila wiki.
Akizungumza baada ya kupata washindi wa wiki ya
kwanza ya awamu ya pili juzi, Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel
Tanzania, Hawa Bayuni alisema zaidi ya Sh324 zilitengwa kama zawadi ya
fedha taslimu kwa ajili ya promosheni na mwenendo wa idadi ya pointi za
washiriki unazidi kutia hamasa.
“Mwenendo wa washiriki wa Mimi ni Bingwa kuendelea
kujikusanyia alama unazidi kuvutia. Watu wengi wameona wakicheza zaidi
wanajikusanyia alama Zaidi, hivyo kujiongezea nafasi zao za ushindi bado
kuna zawadi nyingi, ikiwamo zawadi kubwa ya Sh50 milioni,” alisema
Bayuni.
Mmoja wa washindi wa droo ya wiki hii, Saidi
Kitambuliyo, alishukuru Airtel kwa kumsaidia kuanza mwaka kwa kishindo.
“Fedha hizi zimekuja wakati mwafaka… bahati nasibu iliyoruhusiwa na
Serikali ni sawa na uwekezaji,” alisema.
Pia, Bayuni alisema washindi wa tiketi watapata fursa ya kuchagua mtu mmoja atakayeongozana naye kufurahia safari hiyo.


