Nikiwa muumini mkubwa wa demokrsia na uwazi napata shida kubwa kuamini kama kweli akifanyacho Zitto kwa chama chake kwa sasa ni sahihi. Napata ugumu kumuelewa mwanasiasa huyu machachari wa siasa za kisasa kama kweli anaisimamia misingi ya uwazi na kweli kama inavosema katiba ya chama chake (CHADEMA).
Inaniwia ugumu kumuelewa Zitto kabwe kama kweli anatumia akili yake ya kisomi kutenda anayoyatenda kwa sasa dhidi ya chama chake kwa sasa. Haiwezekani katibu wa chama chake afanye ziara ya kujenga chama kwenye majimbo alafu yeye anatoka nyuma na kupita kila alipopita Slaa tena kibaya zaidi katiba hotuba zake anakikashifu chama chake na viongozi kwa kuwaita majina mabaya ya WAHAFIDHINA. Zitto akumbuke kuwa chama hiki ndicho kimemefanya ajulikane na kuwa maarufu, asiwe mtu wa kufanya vitu kwa utoto.
Jiulize ni kwamba Zitto haijui misingi ya kupata haki ndani ya chama chake?
Je ni kwamba haijui vizuri katiba yake?
Je ni kwamba haamini kama atapata haki yake ndani ya chama akiifata sheria na kanuini za chama?
Nakuwa na maswali mengi ya kujiuliza juu ya kijana huyu, ni kwa nini mikutano yake anayoifanya inaandaliwa na UVCCM?? Akina Mtela Mwampamba, na yule kijana mwingien aliefukuzwa uanachama Habib Mchange??? Ni kwa nini anashirikiana bega kwa bega na vijana hawa wa CCM?? Ni kwa nini ziara yake na mikutano yake haileengi kukijenga chama chake bali kukibomoa??
Zitto ameamua kuanzisah ligi dhidi ya viongozi wakuu wa chama chake na hii hatomusaidia kisiasa na totally itamumaliza, mfano mkutano alioufanya tarehe 23/12/2013 kigoma mini tangu mwanzo hadi mwisho alikuwa anaongelea uongozi wa chama chake kitu amabacho ihatari kwake na chama chake amabacho anajinasibu kukipenda sana!
Nilicho draw sasa ni kuwa Zitto anataka kujisafisaha na kuonekana msafi mbele ya wapiga kura na wanachama wa Chadema kube ni mchafu asieweza kusafishika,
Movement aliyoianzisha sasa chini ya mwanvuli wa DEMOKRASIA itamumaliza kisiasa itamfnya aonekane mhuni na mpenda madaraka kitu amabcho sio kizuri kwake na future yake.
KWA NINI ZITTO SIO MTU MZURI?
1. Anapenda kuonekana msaf sana mbele ya umma kitu amabcaho sio sahihi na pia amekuwa mbinafsi mno.... jiulizeni Zitto hajashiriki kwenye movement za kichama kwa mda mrefu bali amekuwa akijitungia ziara zake ambazo hazijabarikiwa na chama.. huu ni umimi na ubinafsi wa hali ya juu.. Fatilia katiba ya chama chake ukurasa wa 97 .. 6b WAJIBU WA MBUNGE KWA CHAMA
kushiriki moja kwa moja katika ziara za uenezi na ujenzi wa chama kadri zitakavyopangwa na chama....
kila ziara lazima ibarikiwe na ipangwe na chama aache ubinafsi kijana huyu
Ni ngumu yeye kutuminisha kuwa alikuwa busy sana kiasi cha kutoshiriki kwenye movement hizi
2. Kwani Zitto hajui kwamba anachokifanya sasa kinaweza muondoa uanachama wake?? kwani jhajui kwamba kama kiongozi aliepita kukisoa chama chake mbele ya umma ni kosa kubwa??
wengi wameongea kuhusu yeye kutopeperusha bebdera ya chama chake katika mikutano yake ilihali anaongea mambo ya CHADEMA. Wengi wamehoji na majibu mepesi tu ndo yametolewa kuwa Chama hakina pesa ya kununulia bendera, hii ni akili ndogos ana na hahitaji kufikiraia na kuuliza maswali. Anasema anafanya ziara ya chama na hana bendera ya chama.. huu ni totally Uongo
Hakuna lie juu ya chama chake hapa Tanzania na duniani kote, walikuwepo wanasiasa mahiri zaidi ya Zitto lakini sasa wako wapi, walikuwa wakidahni wangeweza kusimama na kuendeleza umaarufu wao hata baada ya kutoka kwenye vyama vyao lakini walipotea Mfano Augostino Lyatonga Mrema, aliondoka CCM akidhani yeye ni maarufu zaidi ya Chama chake kumbe haikuwa hivo. akina prof. Kigoma Malima ni mifano ya wanasiasa wachache tu
Zitto ajiangalie sna asije kuingia kwenye mkubo na shimo la sahau walilopitia wanasiasa hawa, namshauri ajitazame upya na aangalie upande mwema asije kupotea.