National
Geographic ya Washington, DC siku ya Jumatano, Dec 11, 2913 walionyesha
vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye mbuga zetu za wanyama kwa
wahudhuriaji ambao wengi wao walikua Wamarekani pia ulialikwa Ubalozi
wa Tanzania akiwemo Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia,
Mhe. January Makamba.

Mhe.
January Makamba akitoa shukurani zake kwa National Geographic kwa
jitihada zao za kusaidia kutangaza hifadhi za Taifa za wanyama pori.

Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwapongeza
National Geographic kwa kuwa Mabalozi wa Tanzania nchini Marekani na
kuahidi kufanya nao kazi kwa karibu zaidi na mlango wa Ubalozi wa
Tanzania upo wazi pindi wanapohitaji msaada.

Mkurugenzi
Mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi nae akiwapongeza
National Geographic kwa jitihada zao za kutangaza mbuga za wanyama pia
aliwahakikishia wahudhuriaji Tanzania ndio mahali pekee kwenye vivutio
na aina nyingi ya wanyama hao.
Andrew
Evans mfanyakazi wa National Geographic ambaye ndiye aliyetembelea
mbuh=ga za wanyama Tanzania, akiwaonyesha wahudhuriaji picha mbalimbali
za wanyama na kuwaelezea kuhusu Tanzania kwamba ni nchi ya Amani na
Utulivu na Watanzania waliojaa na upendo kwa kila mtu.
Akianza kuelezea alianza kuwaonyesha Khanga kwamba hutumika kwenye shughuli nyingi na kwamba utaiona kila pahala.
Pia
alionyesha picha ya kukutana na marafiki zake hao kwenye picha na yeye
alipewa jina la Mzungu, Andrew Evans anaufahamu mkubwa wa hifadhi za
Taifa jinsi alivyozielezea na vitu vilivyomo lazima uatatamani kuelekea
huko kesho.

Mhe.
Balozi Liberata Mulamula na Mhe. January Makamba wakiongea na
wahudhuriaji walijaribu kudadisi mambo mengine kutoka Tanzania na
kuahidi kuja nchini Tanzania kutembelea mbuga za wanyama.

Mhe.
January Makmba akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe.
Liberata Mulamula ndani ya thieta za National Geographic, Washington,
DC.

Kutoka
kushoto mstari wa mbele ni Afisa wa Ubalozi Mindi Kasiga, Mkurugenzi
mkuu wa Tanzania National Parks, Bwn. Allan Kijazi, Naibu Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba na Balozi wa
Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula katika picha ya pamoja
na wahudhuriaji wengine waliofika National Geographic ya Washington, DC.
(Picha kwa hisani ya Vijimambo Blog)