Wakazi nane wa Dodoma watimka na bodaboda za Vodacom

Picture
Kaimu Meneja Masoko wa Vodacom Kanda ya Kati, Heladius Kisiwani (Wapili kulia), akiwa ameshikana mikono na washindi wa promosheni ya "Timka na Bodaboda" mara baada ya kuwakabidhi pikipiki wakazi wanane wa mkoani Dodoma.
Dodoma... Huku maisha ya mamia ya watanzania yakiendelea kuboreshwa kupitia promosheni ya Timka na  Boda Boda inayoendeshwa na kampuni inayoongoza kwa mawasiliano hapa nchini ya Vodacom Tanzania,Safari hii wakazi wa kanda ya kati wameshuhudia washindi nane wa promosheni hiyo wakikabidhiwa bodaboda zao.


Promosheni hiyo yenye mafanikio makubwa na kupendwa na idadi kubwa ya watu imekuwa ikitoa bodaboda tano kila siku na fedha taslimu kiasi cha milioni moja kwa washindi wake na kuendelea kushika kasi kwa kubadilisha maisha ya wateja wa
kampuni hiyo ambapo mpaka sasa zaidi ya 200 wamejishindia Pikipiki na 90 wamejishindia pesa taslimu nchi nzima.

Akizungumza na waandishi Habari wakati wa kuwakabidhi washindi hao  Kaimu Mkuu wa kanda ya kati Kisiwani Laurent alisema kwamba yeye kama mwakilishi wa Vodacom anafurahi sana kuona kampuni yake inatimiza yale ambayo imekusudia na kubadilisha maisha ya wateja wake kuwa na ndoto za maendeleo na kiuchumi,kwani najisikia faraja sana kuona wateja wetu wanakuwa na maendeleo.

"Huu ni utamaduni wa promosheni hii ya timka na bodaboda wa kila mteja wake aliejishindia pikipiki kupelekewa popote pale aliko,Promosheni hii imelenga kuwanufaisha zaidi wateja wetu kujikwamua kiuchumi kwa kuwaongezea mitaji yao na kuwawezesha kufanya biashara na kujiongezea vipato kupitia biashara zao wenyewe."

 "Wote tunajua kuwa sasa Bodaboda ndio habari ya mjini, kulingana na mfumo wa maisha ya sasa. Napenda kutoa wito sana  kwa wateja wote wa mkoa huu wa Dodoma waendelee kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma Neno PROMO kwenda namba 15544. Alisema  Kisiwani