ZITTO ATOA VIJEMBE VIKALI!!!


 Siku moja mume na mke wake walifunga safari kwenda kijiji jirani.
Mume akamwambia mke wake apande punda yeye akaenda akiishikilia kamba.

Wakakutana na wakulima wanaenda shamba.
Wakulima wakanongonezana: kweli huyu mume bwege! Yeye atembee kwa mguu, mke wake apande punda wakati punda wake mwenyewe. Wakamcheka. Yule mwanamke kwa roho yake nzuri na kwa mapenzi kwa mume wake akasema basi mume wangu panda wewe, mi nitembee majirani wasikucheke.

Mume akapanda punda, mke wake akawa anamfuata nyuma. Wakakutana na wanawake wanaenda kuchota maji. Wanawake wakasema khaaaa! Yaani wanaume wanavyo jipenda hawana mfano! Huyu mwanaume ana nguvu kuliko mke wake ila yeye anapanda punda mke wake anamwacha atembee kwa mguu! Yule mwanaume akasema: ndio maana toka mwanzo nilitaka wewe upande mke wangu maana nawajua hawa wanawake, watatusema sana. Mke akasema: basi tupande wote



Wakaendelea na safari wote juu ya punda, mume kakaa mbele, mke wake kakaa nyuma anamshikilia kiunoni. Wakakutana na wavuvi wanatoka kazini. Wavuvi wakawaambia: hivi huyu punda mnamtendea haki? Yaani uzito wa nyinyi wote wawili na safari yote hii mbona hamna huruma? Wakaona aibu wote wakashuka. Mume akashika kamba ya punda akawa anatembea mbele, mke anamfuata nyuma.

Wakakutana na wawindaji. Wawindaji hawakuwaambia kitu ila tu wakaangusha kicheko. Eti: hivi hawa wanandoa wana akili kweli? Wana safari ndefu, wana punda, ila wanaenda kwa miguu! Si bora wangemwacha punda kwao tu sasa?

Mwanadamu hata ufanye nini huwezi kuwaridhisha watu wote kwa pamoja. watu watasema tu. Ila kama unafanya sababu unajua unacho kifanya na unaamini upo sahihi, watu watakapo sema hutoyumba. Utajua kwanini umefanya hivo na kwanini wanakosea wanapojaribu kutafsiri matendo yako