|
Ofisa
uhusino na masoko wa Mpango wa Taifa wa damu salama Bw. Rajab Mwenda
(kulia) akielezea kuhusu ripoti ya akusanyo ya damu ya robo mwaka na
mikakati ya kukusanya damu kipindi cha Novemba- Januari 2013 wakati
wanafunzi wakiwa likizo
|
Na Mwandishi Wetu
MPANGO wa Taifa wa Damu Salama
Tanzania (NBTS) umevuka malengo ya ukusanyaji damu kwa asilimia
110 katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba 2013 ambapo
jumla ya chupa 38,552 zilikusanywa na kuvuka malengo ya chupa 35,000
zilizokuwa zikusanywe.
Ofisa
Uhusiano na Masoko wa Mpango wa Damu Salama Tanzania Bw. Rajab Mwenda
alisema Kanda iliyongoza kwa makusanyo ya damu ni Kanda ya Mashariki
inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Dodoma na Pwani ambako
jumla ya chupa 13,669 zilikusanywa, Kanda inayofuatia kwa ukusanyaji
damu ni Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro,Arusha, Manyara,
Tanga) iliyokusanya chupa 6,159.
Alisema
katika kipindi cha mwezi oktoba 2012 hadi Septemba 2013 takwimu
zinaonyesha chupa za damu 139,676 ambayo ni sawa na asilimia 99.8 ya
lengo la kukusanya chupa 140,000 ilifikiwa hata hivyo Mpango wa Taifa wa
damu salama unakusanya asilimia 26 ya mahitaji ya damu kwa
mwaka. Mahitaji ya damu kwa mwaka ni wastani wa chupa 400,000- 450,000.
Alisema
tofauti iliyoko ya upatikanaji wa damu kwenye hospitali nchini imekuwa
inafidiwa na ndugu wa wagonjwa katika kuchangia damu ili kuokoa maisha
ya mgonjwa.
Bw.
Mwenda alisema mbalimbali ambazo zinasababisha mpango kushindwa
kukusanya damu kwa 100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari kunatoakana
na uelewa mdogo katika jamii kuhusu uchangiaji damu kwa hiari kwani mfumo uliozoeleka ni ndugu wa mgonjwa ndiyo wanatoa.
Alisema
nyingine ni uhamasishaji usiotosheleza toka kwa viongozi mbalimbali wa
jamii, wanasiasa, viongozi wa dini, uuzwaji wa damu usio halali
hospitalini jambo ambalo linawakatisha tamaa wachangia damu wa hiari,
matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali na miundombinu hafifu
hususan barabara duni wakati wa kukusanya na kusambaza damu.
Bw.
Mwenda alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama una wadau mbalimbali
ambao hujitokeza kuchangia damu kwa hiari kama taasisi za kidini,
majeshi, sehemu za kazi, mikusanyiko ya watu na wanafunzi ambao
huchangia asilimia 80 ya damu hapa nchini
Alisema
katika kipindi cha Novemba hadi Januari kila mwaka ni kigumu katika
ukusanyaji damu kwani wadau wakuu ambao ni wanafunzi wanakuwa likizo ya
mwaka hivyo Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka mikakati mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Alisema katika mikakati hiyo ni kufanya kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu kwa hiari katika jamii na sehemu za makanisani, minadani, stendi za mabasi, misikitini, kwenye masoko na sehemu za kazi.
Alisema
wameanza kuhamasisha kambi za jeshi, makundi ya dini na ma wasiliano
yamefanyika kwa jumuiya mbalimbali hapa nchini zichangie damu mfano
jumuiya ya Khoja shia, Sabato na Jaula.
Pia
alisema watatumia vyombo vya habari ili kuikumbusha na kuielimisha
jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu na visaidie kutoa elimu na
kutangaza ratiba ya ukusanyaji damu katika vituo vidogo na vikuu.
Alitoa rai
kwa Watanzania kujitokeza kuchangia damu kwa hiari katika vituo vya
damu salama kwa mtu yoyote mwenye afya mwanamke au mwanaume na mwenye
umri kuanzia miaka 18 ajitokeze kuchangie damu.
Alisema uchangiaji
wa damu kwa hiari una faida kwa mtoaji kwa vile napunguza hatari ya
magonjwa ya moyo, kuwepo kwa madini chuma mengi kupita kiasi katika damu
kunakodhoofisha utendaji kazi na kuchangia damu mara kwa mara
hurekebisha madini chuma ya ziada katika mfumo wa damu.
Alisema
faida nyingine ni upimaji wa afya pasipo gharama kwa sababu wakati
unapochangia damu mtaalamu wa tiba daktari au muuguzi atapima shinikizo
la damu yako, mapigo ya moyo na kukufanyia vipimo vya afya bure.
Alisema
kutoa damu kunaongeza utambuzi wa kiwango cha chembe hai nyekundu na
chembe na huchochea uzalishaji wa seli damu mpya na kuwaomba wanahabari
kuendelea kuhamasisha na kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia
damu kwa hiari mara kwa mara kwani ni damu ya mwanadamu pekee inayotumika kumuongezea mgonjwa anayehitaji damu.