Namkariri Spika Anne Makinda akisema ‘itakumbukwa hii ni mara ya pili kwa Rais kutuhutubia sisi na tuna utaratibu wa Mihimili kwa hiyo hoja hii naomba tutengue kifungu cha wageni wasiokua wabunge wasiingie humu ndani sasa, hawa tuwakaribishe’
Baada ya hiyo sentensi, Spika aliuliza maswali ya wanaounga mkono na wasiounga mkono ambapo japo kuna waliosema sioo, waliotoa jibu la ndio ndio walishinda kutokana na wingi wao