Kuna mtindo umeibuka wa watu kuwasemea wenzao mitandaoni bila ridhaa
yao. Mimi ni moja ya waathirika wa kusemewa mambo. Sasa kuna mwana JF
kaanzisha kampeni ya kutaka mimi Kitila Mkumbo niwe Katibu Mkuu wa
Chadema. Ujumbe wangu ni kwamba: Vijana acheni kufanya hizi siasa za
bei rahisi. Utaratibu wa kumpata Katibu Mkuu ...wa
CDM unajulikana na hii ya kupigiana kampeni kwenye mitandao sio
mojawapo. Mnaleta mijadala ambayo haipaswi kuwepo na kusababisha
mitafaruku isiyo na maana na kupoteza muda wa kuidhoofisha CCM. Nina
kazi kubwa ya kuelimisha vijana wetu katika vyuo vikuu na ninaifurahia
kazi hii. Mchango mdogo ninaotoa kwa CDM kwa nafasi niliyo nayo sasa
unatosha na ninaridhika.