Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa
NCCR-Mageuzi, Dk Sengodo Mvungi amefariki dunia leo alasiri nchini
Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu
wanaosadikiwa ni majambazi.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti Taifa wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.
Dk
Mvungi ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba
alijeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kichwani Novemba 13, mwaka huu
nyumbani kwake Kibamba Msakuzi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na
kulazwa Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (Moi) na baadaye kuhamishiwa
Hospitali ya Milpark, Johannesbarg, Afrika Kusini.