WAZIRI MKUU MSTAAFU MZEE MSUYA AJITOA KATIKA SIASA; JK AMPONGEZA

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA, JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIWA VIONGOZI WENGINE WAKUU WA SERIKALI CHAMA CHA MAPINDUZI CCM, AKIWEMO KATIBU MKUU WA CCM TAIFA, ABDULRAHMAN KINANA (KUSHOTO) KATIKA HAFLA YA KUMUAGA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA MARA MBILI KATIKA AWAMU MBILI TOFAUTI, MZEE CLEOPA DAVID MSUYA (WA KWANZA KULIA KWA RAIS) AMBAYE AMESTAAFU RASMI SIASA BAADA YA KUITUMIKIA KWA ZAIDI YA MIAKA 33.

 Katibu wa CCM, wilaya ya Mwanga, akisoma historia fupi ya Mzee Msuya kabla na baada ya kujiunga na siasa
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM wilaya ya Mwanga leo
Mjumbe wa Halmashauri kuu wa CCM wilaya ya Mwanga, Joseph Thadayo akitoa salamu za marafiki na wasomi waishio nje ya Mwanga, ikiwemo salamu za Mwanasiasa maarufu na mdhamini wa CCM, Mzee Peter Kisumo ambaye aliwahi kufanya kazi pamoja na mzee Msuya katika Siasa. 
Mzee Msuya akitoa pongezi zake kabla ya kuaga rasmi.

Kundi la wazee wa kimila wakiongozwa na Mzee Kasim Msemo wakimkaribisha Mzee Msuya kijijini
 Mzee Msuya akiwa amekaa kwenye kiti cha jadi kama ishara ya kurudi rasmi kijijini baada kutangaza kustaafu siasa 
 Rais Kikwete akizungumza na wananchi katika hafla ya kumuaga Mzee Msuya katika ulingo wa siasa, uliofanyika leo katika ofisi za CCM wilaya ya Mwanga.
 Mamia ya Wananchi waliokusanyika kushuhudia hafla hiyo

MATUKIO MBALIMBALI YA ZIARA YA RAIS JAKAYA KIKWETE MKOANI KILIMANJARO HAYA HAPA
















Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi waliofika ikulu ya Moshi. 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akizungumza mara baada ya rais kuwasili ikulu mjini Moshi kwa ajili ya ziara wilayani Mwanga .









Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama na serikali.

Baadhi ya wageni wakisalimiana

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi Liberatus Sabas akiteta jambo na mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi Moshi ,Matanga Mbushi. Picha Na Dixon Busagaga

picha IKIONESHA JINSI DARAJA LA BARABARA YA BAGAMOYO LILIVYOKUWA LINAVUNJIKA


Angalia Video Hapa Chini Jinsi Daraja la Mpiji hapa Maeneo ya Bunju Mpakani mwa Dar na Bagamoyo lilivyokuwa linavunjika...... Watu 10 
wamepoteza maisha jijini Dar es Salaam,huku mawasiliano kati ya jiji la Dar-Es-Salaam na wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani yakisimama kwa zaidi ya siku tatu,mara baada ya tuta la barabara pembezoni mwa daraja la mto Mpiji kusombwa na maji umbali wa mita arobani na kuleta adha kwa wananchi wanao tumia barabara hiyo.

Zitto ataka TBC kuchunguzwa


Matangazo hayo yaliyokuwa yanarushwa na TBC1 wakati Tundu Lissu akiwasilisha maoni ya walio wachache katika Kamati Namba 4, yalikatishwa ghafla na kumlazimu mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta kuahirisha kikao hadi leo.
Wakati Zitto akipendekeza kufanyika kwa uchunguzi huo, Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetaka kuwapo uthibitisho wa kitaalamu uliosababisha kukatika kwa matangazo hayo.
Hata hivyo, meneja matukio wa TBC, Mbwilo Kitujime alisema kwa ufupi kuwa hakukuwa na siasa katika suala hilo bali mitambo ilipata hitilafu, lakini akasema kwa ufafanuzi zaidi atafutwe mkurugenzi mkuu wa TBC, Clement Mshana. Mshana hakuweza kupatikana.
Kauli ya Zitto
Akizunguza na gazeti hili kwa simu kutoka nchini India jana, Zitto alisema sababu nyepesi tu kuwa “ni kutokana na hali ya hewa Dar es Salaam” hazikubaliki, hasa kutokana na mwenendo wa TBC.
“TBC inaendeshwa kwa fedha za walipa kodi. TBC ijue kuwa wao si shirika la utangazaji la serikali, bali ni Shirika la Umma. Ni matumizi mabaya ya fedha za umma kuegemea upande mmoja,” alisema.
Zitto, ambaye pia mbunge wa Kigoma Kaskazini na mjumbe wa Bunge hilo, alipendekeza shughuli za TBC kipindi hiki chote cha mjadala wa Katiba ziwekwe chini ya uangalizi wa chombo huru chenye wajumbe kutoka pande zote.
MCT yahoji mfumo
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga alisema mfumo wa sasa wa uendeshaji wa shirika hilo la umma ni mbovu na una kasoro na ndio maana wadau wa habari walipendekeza mabadiliko makubwa katika shirika hilo.
“Kitu kilichotokea jana (juzi) kinathibitisha mambo ambayo tumekuwa tukidai kwamba tutoke kwenye kitu kinachoitwa utangazaji wa serikali twende kwenye utangazaji wa huduma za umma,” alisema.
Kwa mujibu wa Mukajanga, TBC inapaswa kujiendesha kama lilivyo Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), ambalo ni huru likiwa na kasma maalumu na linawajibika moja kwa moja kwa Bunge.
Mukajanga alisema nchi inapokuwa na chombo cha utangazaji cha serikali, watangazaji wanaathiriwa na matakwa ya serikali iliyopo madarakani na ndicho kinachoipata TBC kwa sasa.
Katibu mtendaji huyo alisema watumishi wa TBC hivi sasa wako katika wakati mgumu kupima ama kufanya kazi kwa weledi au kwa matakwa ya serikali baada ya kauli ya Rais Jakaya Kikwete.
“Rais kashasema hadharani anataka serikali mbili, wao (TBC) hawawezi tena kutumia taaluma yao tunayoifahamu ya kuwajibika kwa umma na kutopendelea,” alisisitiza Mukajanga.
Naye mwandishi wa habari wa siku nyingi, Lawrence Kilimwiko alisema hatashangaa kusikia kwamba kukatishwa kwa matangazo hayo kulikuwa ni maelekezo maalumu.
Kilichotokea
Hali hiyo ilitokea juzi baada ya mjumbe wa Bunge hilo, Freeman Mbowe kuomba mwongozo kuhusu TBC1 kusitisha matangazo wakati Lissu akiwasilisha, jambo lililomfanya Sitta kuamua kusitisha shughuli za Bunge.

TAARIFA ZA AWALI KUTOKA CHADEMA KUHUSU MBUNGE WAO ANAYEDAIWA KUMAMATWA AKIGAWA HELA HUKO KALENGA




By Kurugenzi ya Habari: Mbunge wa Viti Maalum, Rose Kamili alikuwa akifanya kikao cha ndani Kijiji cha Kitawaya, Kata ya Luhota, ghafla yeye pamoja name makamanda wengine wanawake aliokuwa nao pamoja wakazingirwa na kikosi cha Green Guard vijana wa CCM.

Wakaanza kumpiga na kumdhalilisha vibaya kisha wakampeleka ofisi za CCM Mkoa wa Iringa kwa maelekezo ya viongozi wao kitaifa na mkoa waliokuwa kwenye mkutano wao was kufunga uliofanyika eneo la Kidamali.

Sasa baadae wakagundua kuwa suala hilo litakuwa gumu kwao ndiyo ikatungwa hiyo propaganda ya kwamba wamemkata kwa rushwa il I wajenge uhalali wa kumpiga na udhalilishaji waliomfanyia.

Polisi walienda kumchukua Mama Kammili akiwa ofisi ya CCM Mkoa ambako walikuwa wakiendelea kumdhalilisha.

Tunafuatilia kwa makini na kina suala hili na tutaendelea kuwapatia taarifa.

CCM iko kwenye wakati mgumu sana wa kukabiliana na ukweli wa kushindwa uchaguzi was Kalenga na kukataliwa na wananchi mchana name usiku.

Ni sawa na mtu anayetapatapa kufa maji.

ORODHA YA MAJINA YA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WENYE ELIMU YA SHAHADA MWAKA 2013/14 -ORODHA YA PILI

faridid zone
ORODHA YA MAJINA YA AJIRA MPYA  ZA WALIMU WA SHULE ZA SEKONDARI WENYE ELIMU YA SHAHADA MWAKA 2013/14 -ORODHA YA PILI.


 Kwa wale walioshindwa kufungua au ku download

Hizi ni nafasi mpya za kazi toka Access Bank....Work Experience haihitajiki, Mwisho wa kuomba ni tarehe 11 mwezi huu


AccessBank Tanzania is a full commercial bank providing micro, small and medium-sized enterprises (MSMEs) with a broad range of appropriate financial services. Established in 2007, the bank is owned by a multinational shareholder group and member of an emerging global network of commercial microfinance banks (the “Access Group”) with headquarters in Berlin/Germany.