Mwasisi wa Chadema,Edwin Mtei amesema kuna baadhi ya watu nchini wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanafanya njama za kukidhoofisha na hata kukipoteza kabisa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mtei,alitoa
kauli hiyo wakati chama hicho kikiwa katika wakati mgumu baada ya
baadhi ya viongozi wake kushambuliana kupitia mitandao ya kijamii, huku
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha,Samson Mwigamba
akisimamishwa kwa madai ya kukiuka kanuni za chama hicho.
Akihojiwa
na gazeti hili, Mtei alisema kuna baadhi ya watu kutoka Chama Tawala
cha CCM wanahakikisha wanatengeneza mifarakano kila kukicha ili
kukivuruga Chadema.
Alisema
mara baada ya Rais Jakaya Kikwete kutoa kauli kuwa huenda CCM ikang”oka
mwaka 2015, baadhi ya makada na viongozi wameanza kukesha wakifanya
mbinu ya kukivuruga ili Chadema kisishike dola.
“Kuna watu wa CCM wanakesha usiku na mchana kuhakikisha wanatuvuruga, ili tusishike dola mimi nasema hawatuwezi”alisema Mtei
Hatahivyo,alisema
kitendo cha kusimamishwa na hata kufukuzwa baadhi ya makada wa Chadema
kimetokana na usaliti ndani ya chama hicho huku wengine wakikubali
kutumiwa na CCM.