HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA ZITTO KABWE KWENYE AKAUNTI YAKE YA FB MDA MFUPI ULIOPITA.........

Mwisho wa uongo ni aibu. Siasa za uongo hazilipi. Lazima mtu mmoja ajitoe muhanga kukomesha siasa za uongo na utungaji hekaya. Nimeamua kuchukua wajibu huo kuokoa nchi kutoka kwenye makucha ya siasa za uongo, uzushi na uzandiki. Iwe fundisho kwa vifaranga na mama zao. Mabadiliko ni hoja na kusimamia hoja za umma na sio utungaji wa hekaya dhidi ya washindani wako kisiasa.